Donald Trump atangaza kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Syria

Rais wa Marekani Donald Trump ameshangaza kila mtu wengi siku ya Jumanne, Mei 13, kwa kutangaza kutoka Riyadh, nchini Saudi Arabia, kwamba anaondoa vikwazo vya Marekani dhidi ya Syria, katika mkesha wa mkutano wake na Rais wa mpito wa Syria Ahmed Al-sharaa nchini Saudi Arabia.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

“Nitaagiza kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Syria ili kuwapa nafasi ya ukuu,” rais wa Marekani amesema, akionyesha kuwa amefikia uamuzi huu baada ya maombi ya haraka kutoka kwa mwenyeji wake, Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Assaad al-Shaibani amekaribisha uamuzi huo wa rais wa Marekani, na kuutaja kuwa “mabadiliko madhubuti” kwa nchi yake. Akinukuliwa na shirika rasmi la habari la Syria SANA, Assaad al-Shaibani ameonyesha kwamba kuondolewa huku kwa vikwazo vya Marekani kunakuja wakati Syria inakwenda “kuelekea mustakabali wa utulivu, utoshelevu na ujenzi wa kweli baada ya miaka mingi ya vita haribifu.”

Donald Trump ameshangaza wengi kwa kutoa tangazo hili katika mkesha wa mkutano uliopangwa kufanyika siku ya Jumatano, Mei 14, nchini Saudi Arabia na Rais Ahmed Al-sharaa. Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani alisema muda mfupi kabla ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo kwamba rais wa Marekani “amekubali kusalimiana” na rais wa mpito wa Syria, ambaye amekuwa madarakani tangu kuanguka kwa Bashar Al Assad mwishoni mwa mwaka 2024.

Bilionea huyo wa kihafidhina amekiri kufanya uamuzi huo baada ya maombi ya mara kwa mara kutoka kwa Mohammed bin Salman. Akiwa amekaribishwa kwa fahari kubwa mjini Riyadh, Donald Trump hakukosa kumsifu mzungumzaji wake wa Saudia. ” Nini sintofanya kwa Mwanamfalme,” amesema.

“Tumekuwa na matangazo kadhaa …”

Katika mitaa ya Damascus, ambako uchumi umekuwa ukisuasua kwa zaidi ya muongo mmoja, tangazo la Marekani linasikika kama mwanga wa matumaini, anabainisha mwandishi wetu, Mohamed Errami. Kwa wengi, kuondolewa kwa vikwazo kunaweza hatimaye kufufua ujenzi uliokwama na kupunguza mzigo wa taabu za kila siku. “Kabla ya mwaka 2011, hakukuwa na vikwazo. Tulikuwa na kila kitu nchini. Tulikuwa nchi ambayo hatukukosa chochote. Ikiwa kweli wataondoa vikwazo, ni wazi hali itakuwa bora zaidi katika ngazi ya kijamii, kiuchumi na kitalii. Lakini juu ya yote, serikali lazima ifanye jambo moja muhimu sana: kutekeleza sheria na kuhakikisha kwamba kila mtu yuko chini yake kwa njia sawa,” Ahmed, mfanyabiashara, amemwambia mwandishi wa habari wa Mohamed huko wa Damascus.

Shauku inasalia kuwa angalifu katika mji mkuu wa Syria, ambapo watu wamejifunza kuwa waangalifu. Jamal, mhudumu katika chumba cha chai katika mji mkongwe, anafahamu kwamba hata kama tangazo hili ni habari njema, itachukua angalau miezi kadhaa kabla ya kuona athari zake halisi katika maisha ya kila siku: “Tumekuwa na matangazo mengi. Lakini ikiwa vikwazo vitaondolewa kweli … Tunachotarajia ni kwamba iandikwe rasmi na kwamba isibadilike.”

Tangazo la Donald Trump limewashangaza wengi huko Damascus. Inabakia kuonekana ikiwa mkutano wa Riyadh na Rais Ahmed Al-Sharaa utaashiria mabadiliko, au itakuwa sehemu nyingine tu katika historia ndefu ya matumaini yaliyopotea. Wakati huo huo, huko Damascus, watu wanatazama – bila matumaini makubwa – kwa dalili za kwanza za mabadiliko ya kweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *