Donald Trump anasema ‘hafanyi mzaha’ anapozungumzia kuhusu kugombea muhula wa tatu

Rais wa Marekani Donald Trump amehakikisha katika mahojiano yaliyofanywa hadharani Jumapili, Machi 30, kwamba “hafanyi mzaha” aliporejelea kwamba anafikiria kugombea muhula wa tatu wa urais, jambo ambalo linapigwa marufuku na Katiba ya Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Sifanyi mzaha,” rais wa Marekani amehakikishia wakati wa mahojiano ya simu na NBC. “Kuna mbinu za kufanya hivi,” ameongeza, akihakikisha kwamba “watu wengi wanataka (yeye) afanye hivi.” Ameongeza kuwa kwa sasa “ni mapema sana kufikiria juu ya hilo.”

Alipoulizwa na NBC kuhusu hali inayowezekana ambapo Makamu wa Rais JD Vance aligombea urais na kisha akatoa nafasi kwa Donald Trump, rais huyo wa Marekani alijibu kuwa hiyo ni mbinu “moja”, akiongeza kuwa “kulikuwa na nyingine.”

Hii si mara ya kwanza kwa Donald Trump, ambaye ndio kwanza ameanza muhula wake wa pili baada ya kuwa tayari rais kati ya mwaka 2017 na 2021, kutoa maoni kama haya. Mwezi wa Januari mwaka huu, alisema “hakujua” kama alizuiwa kuwania tena urais. Kwa mujibu wa Gazeti la New York Times, aliwaambia wabunge wa chama cha Republican: “Nadhani sitagombea tena isipokuwa mtasema, ‘Yeye ni mzuri sana lazima tutafute njia.'” “Hakuna anayeweza kuchaguliwa zaidi ya mara mbili kwenye kiti cha rais.”

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 78 pia alitoa matamshi yaliyotangazwa sana kwenye mkusanyiko wa Wakristo wahafidhina, akiwaambia “hawatahitaji tena kupiga kura” ikiwa atashinda uchaguzi. Lakini Donald Trump pia alipendekeza kuwa kampeni iliyomrudisha White House itakuwa ya mwisho kwake.

Marekebisho ya 22 ya Katiba, yaliyoidhinishwa mwaka wa 1951, yanasema kuwa “hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kwenye kiti cha Rais.”

Mbunge wa chama cha Republican kutoka Tennessee aliwasilisha pendekezo mnamo Januari la kurekebisha Katiba kutoka “mara mbili” hadi “mara tatu,” lakini jaribio hilo linaonekana kushindwa. Kurekebisha Katiba ya Marekani kunahitaji kura ya thuluthi mbili katika Bunge la Congress, jambo ambalo Warepublican wako mbali sana kufikia idadi hiyo, kabla ya kuidhinishwa na angalau majimbo 38 ya Marekani kuna uwezekano mkubwa sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *