Donald Trump amuita Volodymyr Zelensky, ‘dikteta ambaye hakuchaguliwa’

Vita vya maneno kati ya Volodymyr Zelensky na Donald Trump vimfikia kiwango kipya siku ya Jumatano, Februari 19. Kwa kujibu maneno ya rais wa Ukraine kwamba mwanahafidhina huyo wa Marekani “alikuwa “anadanganywa” na Moscow,” Donald Trump amemuita mwenzake “dikteta ambaye hakuchaguliwa” na akamshambulia kwa umaarufu wake na madai ya ubadhirifu.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi kati ya Washington na Kyiv yanazidi kuwa makali. Mahusiano, ambayo yamedorora tangu Marekani kuanza maelewano na Urusi kwa nia ya majadiliano ya kumaliza vita nchini Ukraine – juhudi za kidiplomasia ambazo Ukraine na nchi za Ulaya kwa sasa zimejitenga – na mahusiano hayo yanazidi kuwa mbaya.

Mashambulizi yake yanafuatia kauli ya Zelensky, alivyojibu mazungumzo kati ya Marekani na Urusi huko Saudi Arabia ambapo Kyiv haikushirikishwa, akisema kuwa rais wa Marekani alikuwa “anadanganywa” na Moscow.

Lugha ya “dikteta” ilichochea ukosoaji wa haraka kutoka kwa viongozi wa Ulaya, wakiwemo Kanzlera wa Ujerumani, Olaf Scholz, ambaye alisema, “ni jambo lisilo sahihi na hatari kukanusha uhalali wa kidemokrasia wa Rais Zelensky.”

Lakini saa chache baadaye, bado mnamo Februari 19, Donald Trump alikuwa mkali zaidi kuhusu Volodymyr Zelensky katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao. Kupitia jukwaa lake la Ukweli wa Jamii, rais wa Marekani alimshambulia mwenzake wa Ukraine, “dikteta bila uchaguzi.” “Zelensky anapaswa kufanya haraka au hatakuwa na nchi iliyobaki,” aliandika Trump, ambaye “anaipenda Ukraine, lakini Zelensky amefanya kazi mbaya.”

Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth akimwambia Zelensky kufanya haraka kuingia makubaliano ya kuvimaliza vita ama ajiandae kuipoteza nchi yake. Matamshi yake yanafanana ya yale yaliyowahi kutolewa huko nyuma na Ikulu ya Kremlin kuhusiana na Ukraine na Zelensky. 

Zelensky mwenyewe amemjibu Trump kwa kusema kwa sasa watasimama imara kwa miguu yao na kuongeza kuwa anautegemea umoja wa watu wake, ujasiri na mshikamano na Ulaya. Amesema kupitia iujumbe wa video jana usiku kwamba ana matumaini makubwa na kitakachofikiwa kwenye mazungumzo na mjumbe wa Marekani Keith Kellog.

Baadhi ya viongozi wameyakosoa matamshi hayo ya Trump dhidi ya Zelensky, miongoni mwao akiwa ni Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliyeliambia gazeti la Der Spiegel kwamba ni matamshi potofu na hatari. Amesema ni hatari na si sawa kukana uhalali wa kidemokrasia wa Rais Zelensky, ambaye yuko madarakani kulingana na sheria za nchi hiyo.

Zelensky alichaguliwa mnamo mwaka 2019 kuongoza kwa miaka tano, lakini amesalia madarakani chini ya sheria ya kijeshi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini mwake. Sheria ya Ukraine hairuhusu uchaguzi katika nyakati za vita.