Donald Trump aanza kusambaratisha vyombo vya habari vya Marekani vinavyofanya kazi nje ya nchi

Utawala wa Trump siku ya Jumamosi, Machi 15, 2025, umefuta wafanyakazi wa kituo cha habari cha Sauti ya Amerika (VOA), Radio Free Asia, na vyombo vingine vya habari vinavyofadhiliwa na Marekani na kuibua ukosoaji kutoka kwa watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari ambao wanaona kama kinyume na mfumo wa kidemokrasia kote duniani. Ikulu ya White House imeeleza kuwa hii ina maana kwamba “walipakodi hawapaswi tena kulipia propaganda zenye msimamo mkali.”

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump alitoa dokezo siku ya Ijumaa alipoainisha shirika linalosimamia vyombo hivi vya habari vya umma kama moja ya “vipengele visivyo na maana ya urasimu wa shirikisho.” Agizo hili linaainisha shirika la serikali linalosimamia vyombo hivi vya habari (USAGM) miongoni mwa “vipengele visivyo na maana vya urasimu wa shirikisho.” Baada ya hayo, Kari Lake, mfuasi mkuu wa Donald Trump, ambaye alimteua katika nafasi ya ushauri katika USAGM baada ya kushindwa katika uchaguzi wa maeneti katika jimbo la Arizona, ameandika katika barua pepe kwamba ruzuku ya shirikisho kwa vyombo hivi vya habari “siyo kipaumbele tena” kwa shirika hilo.

Barua pepe ya kutangaza kumalizika kwa mkataba

Baada ya tangazo hilo hatua ya kuwafita kazi wafanyakazi ilifuatiwa, daima kwa njia hii ya kikatili: barua pepe rahisi na mahusiano mara moja hukatwa. Mamia ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine wa VOA, “Voice of America,” Radio Free Asia, Radio Free Europe, na mashirika mengine wamepokea barua pepe mwishoni mwa wiki hii kuwafahamisha kwamba watazuiwa kuingia katika ofisi zao. Pia wanaagizwa kusalimisha kadi zao za vyombo vya habari, simu za kazini na vifaa vingine, anaripoti mwanahabari wetu huko New York, Carrie Nooten.

Mkurugenzi wa VOA mwenyewe amefukuzwa kazi—wafanyakazi wengine wote wana mkataba hadi mwezi Juni—lakini makao makuu ya kituo hiki huko Washington yamefungwa; Hii inasambaratisha redio, ambayo imekuwa sauti ya Marekani kwa ulimwengu tangu mwaka 1942, ikitangaza habari katika lugha 49 kwa wasikilizaji milioni 360 kwa wiki.

Vyombo vya habari kama vile Sauti ya Amerika na Radio Free Asia kwa muda mrefu vimezingatiwa kama “sauti za Amerika” katika nchi ambazo ufikiaji wa habari huru unachukuliwa kuwa mgumu zaidi, kama vile Ulaya Mashariki, Mashariki ya Kati na Asia. Pia ni chombo cha “soft power ” cha Marekani, kama ilivyokuwa kwa Radio Free Europe (iliyozinduliwa mwaka wa 1950) wakati wa Vita Baridi. Vile vile, Radio Free Asia, iliyoanzishwa mwaka 1996, inalenga kutoa ripoti zisizo na uhakiki kutoka kwa nchi ambazo vyombo vya habari haviko huru, zikiwemo China, Burma, Korea Kaskazini na Vietnam.

Rais wa Marekani anaeleza kwa uwazi na mara kwa mara chuki yake kwa vyombo vya habari, ambavyo baadhi yavyo anavitaja kuwa “maadui wa watu.” Kuvunja vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vinavyofanya kazi nje ya nchi kunaweza kukabiliwa na vikwazo kwa sababu Baraza la Congress lina mamlaka ya mwisho, na baadhi ya vyombo, kama vile Radio Free Asia, vimefurahia kuungwa mkono na Wademocrats na Republican hapo awali.

Kamati za Ulinzi wa Waandishi wa Habari zinashangazwa na “zawadi” hii ambayo Donald Trump anatoa kwa tawala za kimabavu za Urusi, China, na Iran – ambazo zinachukia vituo hivi vya redio, ambavyo uandishi wa habari huru ulipinga tawala zao. Hatimaye, wana wasiwasi kuhusu hatima ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika nchi zenye mamlaka, ambao wana hatari ya kufukuzwa mara moja mara tu mkataba wao wa ajira utajkapofutwa.

Tangazo hilo pia limeshutumiwa vikali na mashirika ya uhuru wa vyombo vya habari, linaripoti shirika la habari la AFP. “Inasikitisha kwamba Ikulu ya White House inatafuta kuchokoza chombo kinachofadhiliwa na bunge ambacho kinaunga mkono uandishi wa habari huru ambao unapinga sauti za tawala za kimabavu kote ulimwenguni,” amesema Carlos Martinez de la Serna, afisa wa Kamati ya Kulinda Wanahabari (CPJ). Shirika la Waandishi Wasio na Mipaka (RSF)linasema uamuzi huu “unatishia uhuru wa vyombo vya habari duniani kote na kuharibu miaka 80 ya historia ya Marekani kwa ajili ya mtiririko huru wa habari.”

“Zawadi kubwa kwa maadui wa Marekani,” rais wa Radio Free Europe/Radio Liberty Stephen Capus pia amelalamika katika taarifa yake. “Maayatollah wa Iran, viongozi wa Kikomunisti wa China, na watawala wa kiimla huko Moscow na Minsk wanaweza tu kufurahia kutoweka kwa RFE/RL baada ya miaka 75,” kiongozi huyo, Stephen Capus, amesema katika taarifa.

Sekta ya umma katika njia panda

Donald Trump na mshirika wake mkuu Elon Musk, ambaye anaendesha makampuni kama Tesla, SpaceX, na X, wamechukuwa hatua ya kikatili katika utumishi wote wa umma wa Marekani, wakilenga idara nyingi kama vile Elimu, Afya, na mashirika kama vile USAID, ambayo inasimamia misaada ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *