Dar es Salaam. Februari mwaka huu, Tanzania iliandika historia baada ya Serikali kuongeza likizo yake ya mali¬po ya uzazi kwa wazazi wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti), mabadiliko ya sera ambayo yatanufaisha maelfu ya familia.
Katika Mkutano wa 18, Kikao cha Nne, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Muswa¬da wa Marekebisho ya Sheria ya Kazi (Na.13) wa mwaka 2024, ambao ulifanyia marekebisho kifungu cha 33 ili kuongeza likizo ya uzazi kwa watumishi wanaojifungua watoto njiti, kuruhusu likizo yao ya uzazi kuongezwa ili kujumuisha wiki zilizosalia za wiki 40 za ujauzito.
Pia, Muswada ulioidhinishwa umeongeza muda wa likizo ya uzazi kwa aki¬na baba wenye watoto njiti kutoka siku tatu hadi siku saba. Sheria ya sasa hivi sasa inasomeka hivi: Ikiwa mama atajifungua mtoto njiti kati¬ka wiki 24, atakuwa na haki ya kupata likizo ya uzazi yenye malipo ya miezi tisa (wiki 40—wiki 24) pamoja na nyongeza ya miezi mitatu ya sasa. Na kadhalika.
“Mfanyakazi anayejifungua mtoto njiti ana haki ya kupata likizo ya uzazi yenye malipo kuanzia tarehe ya kujifungua hadi kukamilika kwa wiki arobaini za ujauzito na likizo ya uzazi iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (6) ndani ya mzunguko wa likizo.”
Kila kilicho hai kinastahili kupigania maisha, na Doris Mollel anaibeba imani hii kwa shauku kubwa isiyo na mashaka. Akiwa amezaliwa na wiki 27 tu na uzito wa gramu 900 tu, Doris alipambana na hali hiyo tangu utotoni. Akiwa amekulia katika jamii ambayo watoto njiti wamekuwa wakikabiliwa na unyanyapaa, aliibadilisha historia yake kuwa kiini cha harakati za mabadiliko.
Kupitia mapenzi yake yasiyo na kikomo, Taasisi ya Doris Mollel iliibuka kama mwanga wa matumaini, ikitetea bila kuchoka huduma za afya ya uzazi na mtoto, na kubadilisha mtazamo wa watu kuhusu watoto njiti. Doris anaongoza harakati za masuala ya afya ya mtoto na mama na kubadilisha maisha.
Mwaka 2015, Doris aligundua siri iliyojificha kwa muda mrefu ambayo ilibadili maisha yake. Alifahamu kuhusu kipindi kigumu cha maisha alichokipitia yeye na ndugu yake wakiwa watoto njiti, mapito ambayo kwa kiasi kikubwa yalimpa nguvu ya kutaka kubadili hali iliyopo.
Bila ya kutetereka, Doris alianzisha Taasisi ya Doris Mollel (DMF), akishawishiwa na kauli yake yenye nguvu: “Nikiacha kupigana, watoto njiti watafariki.” Kauli hii si maneno tu ya kawaida; ni ahadi kwa watoto njiti wen-gi walio katika mazingira magumu kote Tanzania na Afrika.
Kwa miaka mingi, DMF imekuwa shirika la kwanza na la pekee kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania kuhusu huduma za watoto njiti na kuongoza mageuzi makubwa ya kisera ambayo hayajawahi kufanywa hapo awali.

Jopo la wadau wa masuala ya watoto njiti wakijadiliana kuhusu nyongeza ya likizo yenye malipo kwa wazazi wanaojifunga watoto njiti na baba wenye watoto njiti katika ukumbi wa Kilimajaro Hyatt Regency mwaka 2018.
Leo, DMF imeajiri wafanyakazi wapatao 11 na imesambaa nchi nzima kwenye mikoa 27 kati ya 30. DMF imeokoa zaidi ya maisha ya watoto 17,000 njiti na kubadilisha moja kwa moja maisha ya maelfu ya vijana, wasicha¬na, vijana na wanawake kupitia programu zake.
“Mafanikio yetu yame¬jengwa kwenye mbinu yenye nguzo kuu tatu: utetezi unao¬tegemea ushahidi, ushaw¬ishi wa sera unaoendeshwa na utafiti, na uhamasishaji unaoongozwa na jamii. Kazi yetu imejikita katika taarifa (data) na utafiti, na kuhaki¬kisha kwamba kila mapende¬kezo ya sera yanaungwa mkono na ushahidi thabiti.
Wakati huo huo, tume¬kuwa tukitoa kipaumbele kwa sauti zisizosikika. Wale walioathiriwa moja kwa moja na changamoto za afya ya uzazi na watoto njiti sio tu wanufaika bali ni washiri¬ki hai katika kuunda masu¬luhisho yetu.
Juni 2018, tulianza ras¬mi. DMF iliitisha semina ya wadau jijini Dar es Salaam kujadili umuhimu wa kuongeza likizo ya wazazi kwa wale wenye watoto njiti; tukio ambalo lilileta pamoja wafanya maamuzi wakuu,” anaeleza Doris.
Majadiliano ya siku hiyo yaliweka msingi wa kile ambacho kingekuwa mapambano ya miaka min¬gi ya kugeuza utetezi kuwa sheria.
“Hatukuwa tu tunakuza uelewa wa watu; tulikuwa tunataka watu wachukue hatua. Miezi michache tu baadaye, Novemba 2018, DMF ilihamishia mapam-bano hayo rasmi Bungeni. Tukiwahutubia wabunge wanawake Bungeni Dodoma, tuliweka bayana umuhimu wa mabadiliko ya sera.
“Watoto njiti, ambao wanakabiliwa na changamo¬to kubwa za kiafya baada ya kuzaliwa, wanahitaji hudu¬ma maalumu na wazazi wanahitaji muda wa kuwapa¬tia huduma hizo. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, mabadiliko ya lik¬izo ya uzazi yalikuwa kwenye ajenda ya kisheria,” anafa¬fanua zaidi Doris.
“Kufikia 2021, tulikuwa tumefikia pazuri, lakini bado mabadiliko ya kweli yalihitaji utashi wa kisiasa. Mwaka huo huo, DMF, kwa ushirikiano na Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Bunge, ilizindua Ajenda ya Watoto Njiti 2021, kampeni ya nchi nzima iliyokuwa iki¬pambania maboresho mata¬tu muhimu ya kisera.
“Watu wengi wanafikiri mapambano yetu yalianza miaka mitatu iliyopita, lak-ini sio kweli. DMF ilianza kupigania mabadiliko ya sera katika eneo la afya ya uzazi na mtoto tangu mwaka 2016. Tangu wakati huo, tume¬ongoza mageuzi makubwa ambayo yameleta mabadi¬liko ya huduma ya afya ya watoto wachanga na akina mama nchini.
“Mwaka wa 2016, tulipigia chapuo uingizaji wa elimu ya watoto njiti katika mtaala wa kitaifa wa sayansi, ili kuhaki¬kisha kwamba vizazi vijavyo vinaelewa changamoto za utoaji huduma na matunzo ya watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
“Kufikia 2020, mapam¬bano yetu yalichukua sura mpya ambapo nguvu ili-hamishiwa katika mabadi¬liko ya huduma za bima ya afya ambayo yalisababisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Chama cha Watoa Bima Tanzania (ATI) kuanza kutoa huduma za matibabu kwa watoto njiti kwa mara ya kwanza nchini. Mwaka 2023, juhudi zetu zil¬isababisha Serikali ya Tanza¬nia kutenga Dola milioni 22.8 kushughulikia changamoto zinazohusiana na watoto njiti.
“Huu ni uwekezaji mkub¬wa zaidi wa umma katika huduma za afya ya watoto wachanga katika historia ya nchi. Mwaka huo huo, elimu ya watoto njiti ilijumuishwa rasmi katika mtaala wa elimu wa Taifa na kuwapa wana¬funzi wa shule za msingi na sekondari ujuzi wa utoaji huduma na matunzo kwa watoto njiti,” anaeleza mua¬sisi huyo wa DMF.
Doris amewashukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango kwa kuunga mko¬no ajenda ya watoto nji¬ti pamoja na washirika, na kukiri kuwa mafanikio hayo yasingewezekana bila msaa¬da wao.
“Mapambano ya haki siku zote sio rahisi, na mabadi¬liko ya kimfumo hayatokei mara moja, lakini siku zote nimeamini kuwa na mwende¬lezo katika kile unachopiga¬nia kunaleta maendeleo,” ameongeza Doris.
“Kwa miaka kumi iliyopita, hakuna shirika lolote lisilo la Kiserikali nchini ambalo limeishawishi Serikali kure¬kebisha sheria nyingi katika eneo hili. Na leo hii, hakuna nchi nyingine barani Afrika ambayo imefanikiwa kupiga¬nia mabadiliko hayo ya kisera. Leo, tunasherehekea ushindi muhimu, lakini kes¬ho, tunarudi kwenye mapam¬bano.”