Dk Biteko awapa vijana ujumbe kuhusu amani

Dares Salaam. Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko amewataka vijana kujifunza umuhimu wa amani kama nyenzo muhimu ya maendeleo.

Pia, amewataka kumpuuza mtu yeyote atakayetokea bila kujali kariba yake, kariba, ukubwa wake, elimu yake au uongozi alionao.

“Akazungumza kwa namna yoyote kuhusu uvunjifu wa amani wa Taifa mtu yule tumpuuze kama hatuwezi kumkemea kwa pamoja tumuambie kuwa amani yetu ndiyo mtaji wetu. Tuilinde kwa gharama kubwa kwa sababu yapo mataifa wanayotamani kuwa na amani hiyo,” amesema Dk Biteko.

Dk Biteko ameitoa kauli hiyo leo Aprili 11, 2025 wakati akifungua kongamano la siku ya kuzaliwa kwa Hayati Julius Nyerere lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini hapa.

Kongamano hilo lilibebwa na kaulimbiu isemayo, Maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika Elimu, Uwekezaji na Ujenzi wa Taifa kwenye Amani kwa Maendeleo ya Watu.

Dk Biteko amesema Hayati alitamani kuona Taifa lenye usawa ambalo watu wanapendana na kuheshimiana, linaljali utu na kuthamini kazi kama kipimo cha utu.

“Leo tunapaswa kuendeleza fikra za mwalimu Nyerere kwa kuwekeza katika sekta ya elimu, kilimo, viwanda, teknolojia na biashara ambavyo ndiyo vinategemewa na wananchi kukuza uchumi jumuishi,” amesema.

Amesema Serikali na sekta binafsi zinapaswa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha uwekezaji unaleta tija kwa wananchi na kutengeneza umoja wa kitaifa na kuondoa umasikini miongoni mwao na kuwavuta Watanzania kwa pamoja na kuwa taita moja.

“Hakuna maendeleo yanayowezekana bila amani, baba wa Taifa aliamini katika mshikamano wa kitaifa na alitufundisha amani si tu kukosekana kwa vita bali hali ya jamii kuishi kwa mshikamo usawa na haki kwa watu wote,” amesema.

Amesema kupitia misingi ya utaifa na umoja, upo uwezekano wa kujenga taifa lenye mshikamano thabiti, licha ya totauti za makabila, dini huku akisema kwa sasa Taifa

linanufaika na amani umoja na upendo kwa sababu Nyerere alipanda mbegu hizo.

Amesema ni vyema kumuenzi baba wa Taifa kwa kuwa na mitazamo inayoweka Watanzania pamoja kama Taifa bila kuangalia makabila, dini, hali za kiuchumi na matabaka mbalimbali ya kijamii.

“Tukiweza kuimarisha haya tutabaki wenye furaha mbali na tukitofautiana kimitazamo tutabaki wenye huzuni,” amesema.

Akimzungumzia Nyerere, Dk Biteko amesema ameandika historia ya kuwa kijana mchapakazi, mpiganiaji wa uhuru, mwanafunzi hodari, kiongozi shupavu aliyetamani wakati wote kuona haki usawa, umoja, amani, utu na maendeleo ya taifa vinashamiri si tu kwa Tanzania bali bara zima la Afrika.

Amesema katika uongozi wake Nyerere alijishughulisha na masuala yote ya kijami, yaliyokuwa kiuchumi na kisiasa katika ngazi zote za taifa na kimataifa na mtu anaweza kusema hakuna nyanja ambayo hakujihusisha nayo.

“Hivyo tunapokutana leo kuyaenzi maisha yake tuna uwanda mpana wa masuala ambayo tunaweza kuyakumbuka kwa sababu hakuna alichoacha,” amesema.

Amesema maono ya baba wa Taifa katika elimu, uwekezaji, na ujenzi wa Taifa lenye amani kwa maendeleo ya watu ni fursa nyingine ya kufanya tafakuri kwa baadhi ya mambo ambayo aliyaamini, kuyaishi na yanaendelea kukumbukwa hadi leo.

“Baba wa taifa hatuko naye leo lakini maisha yake yanaendelea kukumbukwa yanendelea kuenziwa na kongamano hili ni ushahidi mwingine kuwa baba wa Taifa pamoja na kuwa hatupo naye duniani bado anaishi mioyoni mwetu na kwenye fikra zetu ya kuyaenzi yale mema yote aliyoyaenzi na kuyaishi,” amesema.

Amesema elimu Nyerere aliamini kuwa sehemu ya nguzo muhimu za kuleta mendeleo ya watu kwa ujumla.

Amesema aliamini kuwa elimu ni msingi na ukombozi na maendeleo ya taifa, kupitia sera ya elimu ya kujitegemea alisisitiza kuwa elimu ni chombo cha kuleta usawa, ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa na alitamani kuona elimu inampa mwanafunzi maarifa ya kumuwezesha kuchangia mendeleo ya jami yake na si kumtenga na jamii yake.

“Hakuamini katika elimu inayomfanya mtu ajitenge na jamii yake na kujiona veye ni wa daraja fulani hakuiamini na badala yake wasomi wakimaliza shule warudi kuitumikia jamii na kutatua changamoto huku,” amesema.

Kuhusu uwekezaji na maendeleo Dk Biteko amesema alilenga kuimarisha uchumi wa taifa kwa msingi wa usawa uwajibikai wa pamoja.

Amesema mwalimu alisisitiza kuwa uwekezaji ni lazima ulenge wananchi na rasilimali ya taifa itumike kwa ajili ya watu wote na si kikundi cha watu wachache huku akipinga mifumo ya uchumi inayozalisha matabaka na ukosefu wa haki huku akihimiza ujamaa na kuitegemea.

Stephen Wasira ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere amesema Mwalimu Julius Nyerere aliacha amani Tanzania lakini leo kuna kizazi cha wanasiasa wanaodai kuwa wanataka kuvuruga amani kama njia ya kupata wanachotaka.

Aliwaambia kuwa amani inayoonekana imejengwa katika mwamba haiwezi kuvurugwa na mtu yoyote huku akibainisha kuwa amani ya Tanzania italindwa na watanzania wenyewe kwa sababu ni zao la umoja wao.

“Huyu ndiyo Julius Kambarage Nyerere tunayemkumbuka, mwalimu ameunganisha nchi zetu kwa sababu aliamini Afrika inahitaji kuwa moja. Mwalimu alisema katika Bunge la Ghana kuwa bila umoja wa Afrika haina mwelekeo,” amesema Wasira.

Amesema hadi anaenda kaburini Mwalimu Nyerere alimini kuwa umoja ndiyo njia pekee inayoweza kuwafanya waafrika kuwa na nafuu katika bara lao.

“Lakini kazi yake alimaliza, iliyobaki ni ya vizazi vinayofuata, alipanda mbegu ambayo viongozi wa Afrika wa Afrika wanapaswa kuitosha na kuiendeleza,” amesema.

Katika miaka 103 ambayo angetimiza sasa sasa Hayati Nyerere anabaki kuwa kiongozi wa mfano ambaye ni ngumu kumkuta katika sehemu yoyote ya Afrika aliyehudumu kwa miaka 21 lakini alitoka madarakani akiwa hana akaunti ndani wala nje ya nchi

“Labda hi ndiyo sababu Watanzania wanapata tabu sana kumsahau,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *