Tunduru. Diwani wa Mchoteka (ACT-Wazalendo), Seif Dauda na Katibu wa Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, Said Mponda na baadhi ya wanachama wa chama hicho wametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wamesema kazi kubwa inayofanywa na CCM na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumpendekeza Dk Emmanuel Nchimbi kwa wajumbe wa mkutano mkuu kisha kumteua kuwa mgombea mwenza wa urais hawana sababu ya wao kubaki upinzani.
Wanachama hao wapya wa CCM wamesema Dk Nchimbi ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Ruvuma na Katibu Mkuu wa chama hicho ameuheshimisha mkoa huo na wao wanapaswa kumuunga mkono.
Diwani huyo na wenzake wamejiunga leo Jumatano, Aprili 2, 2025 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Uwanja wa Shule ya Mringoti, Wilaya ya Tunduru ikiwa ni siku ya kwanza kati ya tano za ziara yake mkoani humo.

Dk Nchimbi anaanza ziara hiyo ya kwanza na akirejea nyumbani kwao tangu mkutano mkuu wa CCM ulipomteua Rais Samia kuwa mgombea urais na Dk Nchimbi mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Baada ya kupewa fursa ya kuzungumza katika mkutano huo,
Diwani huyo amesema kwa yanayoendelea ameona hana sababu ya kubaki upinzani kwani Serikali imetekeleza mambo mengi ambayo walikuwa wanayapigania.
Amesema kata ya Mchoteka kulikuwa na changamoto ya gari la wagonjwa ambapo Serikali imelipeleka:”Sina sababu ya kubaki huko, najiunga CCM. Hodiiiiiii CCM, naombeni mnipokee.”
Kwa upande wake, Mponda amesema:”Nilikuwa CUF, nikahama kwenda ACT Wazalendo na tulipambana mwaka 2020 tukapata diwani wa Mchoteka, lakini kwa yanayoendelea CCM mimi na wenzangu tumeamua kujiunga na CCM.”
Alichokisema Dk Nchimbi
Baada ya kuwapokea wanachama hao, Dk Nchimbi amesema uamuzi wa kujiunga nao unatokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali na hakuna eneo ambalo halijaguswa.
“Kila sehemu maendeleo yameguswa, hakuna kijiji, mtaa wala kata ambayo haijaguswa kwa miradi ya afya, elimu, maji, nishati, kilimo na au miundombinu,” amesema Dk Nchimbi.
Amesema uhai wa chama upo imara kwa kazi kubwa inayofanywa maeneo mbalimbali na kwa hatua hiyo wako tayari kwenda kwenye uchaguzi mkuu wakiwa kifua mbele.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho amesema chama kinaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani na hilo ndilo limewafanya hata wana ACT Wazalendo kujiunga nao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa.
Changamoto ya ndovu, wanyama wanaoharibu mifugo, maji, migogoro ya ardhi na zinginezo Kanali Ahmed amesema:”Mambo mengi yaliyoelezwa tunayafanyia kazi kwani majibu yake yote yapo.”
Mchungaji Msigwa, Kambaya
Mwanachama wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa amesema kwa hali ilivyo na maendeleo yanayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini, “nchi ipo salama katika mikono ya Chama cha Mapinduzi. Sasa sio watu wanakuja hapa wanasema tuandamane, wakataeni.”
Mchungaji Msigwa aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na wanasiasa wanaotaka kuhamasisha maandamano, “sasa tusikubali na kuwakatae wanasiasa wanaopinda pinda.”
Kada ya CCM ambaye alikuwa CUF akaenda Chadema na sasa yupo CCM, Abdul Kambaya, amesema wanachama wa ACT Wazalendo waliojiunga CCM wametumia maarifa zaidi na siyo sauti kama wanavyofanya wengine.
“CCM inahitaji zaidi kuhudumia wananchi, wao wanataka kushika dola na ndiyo maana wakisimama majukwaani kazi yao kuwasema viongozi vibaya na siyo kueleza watawafanyia nini wananchi na hapo ndipo wanakosea,” amesema.
“Ukitaka kutambua chama chenye uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo usianze kwa kile wanachosema majukwaani, anza na safu ya viongozi wake na hapo ndipo utapata ukweli,” amesema.
Kambaya amesema, “tupo hapa kushindana kwa maarifa siyo sauti, maendeleo ni mchakato siyo amri kama wanavyosimama majukwaani. Unawezaje kudai maendeleo huku hutaki