Katika dunia ya leo, wanawake wanazidi kuchukua nafasi muhimu katika sekta ya fedha, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitawaliwa na wanaume.
Ujumuishaji wa wanawake katika sekta hii umeleta mabadiliko makubwa katika uchumi kuanzia usimamizi wa fedha binafsi, biashara ndogo na za kati, hadi nafasi za juu za uongozi katika taasisi za kifedha.
Ushiriki wa wanawake katika sekta ya fedha unahamasisha ukuaji wa uchumi kwa njia mbalimbali. Utafiti umeonyesha kuwa mataifa yenye usawa wa kijinsia katika uchumi huwa na maendeleo ya haraka zaidi.
Ili kuimarisha ushiriki wao ni muhimu kuendelea kupambana na vikwazo vinavyowakabili, kuhimiza usawa wa kijinsia na kuweka sera zinazowawezesha kushiriki kikamilifu katika kuendeleza sekta hii kama inavyofanya Diamond Trust Bank ambayo imeweka mikakati kabambe kuhakikisha wanawake wanapata nafasi kulingana na uwezo wao.
Katika mahoajiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika ofisini kwake, Meneja Rasilimali Watu wa Diamond Trust Bank, Bi. Catherine Mapundi amesema benki hiyo ina sera nzuri kwa wanawake jambo linalowawesha kufikia ndoto zao na kuchangia ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla.
Sera za maendeleo ya wanawake
Tuna sera kuu mbili ambazo ni; Sera ya fursa sawa ambayo inakataza ubaguzi kulingana na jinsia katika kuajiri, kupandisha vyeo na mambo mengine yote yanayohusiana na ajira.
Sera ya likizo ya uzazi na uzazi ambayo inatuwezesha kutoa maeneo ya kina mama kupumzika ama kunyopnyesha mara baada ya kutoka katika likizo ya uzazi. Pia tunatoa likizo ya uzazi kwa kina baba ili kuwezesha malezi ya pamoja.
Kuhusu idadi ya wanawake waliojiriwa kwenye nafasi mbalimali ndani ya benki hiyo Catherine anasema benki hiyo imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuonge¬za uwakilishi wa wanawake katika ngazi zote za uongozi. “Hivi sasa, asilimia 49 ya wafanyakazi wetu ni wanawake, ambapo kati ya hao, asilimia 14 wako kwenye nafasi za usimamizi na uongozi wa juu.
Programu za mafunzo na ukuzaji ujuzi
Catherine anasema benki imekuwa na programu mbalimbali za mafunzo na kukuza ujuzi zinazo¬lenga kuwasaidia wanawake katika ngazi zote za usimamizi. Programu hizi hushughulikia mahitaji mbalim¬bali kuanzia uelewa wa masuala ya kifedha hadi mafunzo ya juu ya uongozi.

Maryvine Peter, Meneja wa Tawi la DTB Centre.
Baadhi ya programu hizo ni; programu ya maendeleo ya uongozi (uongozi bora, uongozi na ushirikia¬no, uongozi wa juu na mabadiliko), mafunzo ya elimu ya kifedha na uja¬siriamali (UTT, dhamana na akiba) na mafunzo ya kidijitali (wanawake katika teknolojia).
“Tumekuwa tukiendesha pro¬gramu za uongozi na mipango ya maendeleo kwa lengo la kuwaan¬daa wasimamizi wetu wadogo na na mameneja wa kati katika maju¬kumu makubwa zaidi na kujaribu kujenga ujuzi wa uongozi, kufikiri kimkakati, kujiamini na kubadilisha viongozi kutoka kuwa bora hadi ubora wa hali ya juu,” alisema Cath¬erine.
Pia tunawatambua wanawake wanaofanya vizuri katika sekta ya teknolojia na tunalenga kuwapa wa¬fanyakazi wetu ujuzi utakawaweze-sha kuwa washindani pamoja na kujifunza kutoka kwa wengine waliopo katika sekta.
Nafasi za ajira na upandishaji wa vyeo
Catherine anasema Diamond Trust Bank inafuata mfumo unaoz¬ingatia sifa za kuajiri na kupandish¬wa vyeo, kuhakikisha kwamba maamuzi yanazingatia sifa, uzoefu na utendakazi, si jinsia. Wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mi¬chakato ya rasilimali watu ili kubaini na kushughulikia tofauti zozote za kijinsia zinazoweza kujitokeza.
“Tunadumisha uwazi katika mi¬chakato yetu ya upandishaji vyeo, kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wanaelewa vigezo vya kujien-deleza. Kuanzia mwaka 2023 hadi 2025 benki imewapandisha vyeo wanawake 37 katika majukumu mbalimbali ya uongozi,” anasema Catherine.
Aidha kupitia programu yake ya Graduate Management Trainee (GMT) Diamond Trust Bank imeku¬wa ikiwawezesha wahitimu wana¬wake kupata nafasi za ajira ndani ya benki hiyo mara tu baada ya kutoka chuo kwa kuwapa mafunzo ya ku¬wajengea uwezo.
“Kila baada ya miaka miwili tunachukua wahitimu 10 kutoka vyuo mbalimbali nchini na kuwapa mafunzo ya kiungozi katika sekta ya fedha kisha baadaye kuwajiri moja kwa moja,” anasema Catherine.
Juhudi za Diamond Trust Bank katika kuwasaidia wanwake kupa-ta mikopo na usaidizi wa kifedha
Katika kuhakikisha inawaweze¬sha wanawake nje ya benki, Dia¬mond Trust Bank inafanya juhudi mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya kifedha, mikopo na akaunti maalu¬mu ambayo inalenga kuwapa wan¬awake nafasi ya kufanikisha ndoto zao.
“Tuna Akaunti ya Amani, akaunti ya akiba kwa wanawake ambayo in-apatikana kwa TZS na USD. Akaunti hii inalenga kuwawezesha wana-wake kuelekea maisha salama na ya kujitegemea ya benki,” alisema Catherine.
Faida za akaunti hii ni; kupata MasterCard ya bure, ina ushin¬dani wa viwango vya riba, asilimia 5 kwa TZS na asilimia 1 ya Dola za Kimarekani, asilimia 10 ya punguzo la ada za sehemu za kuhifadhia vitu (safe deposit locker) na akaunti ya pamoja kuanzia wanawake wawili.
Ushirikiano wa Diamond Trust Bank na taasisi nyingine
Catherine anasema katika kuhakikisha kuwa wanawafikia Watanzania wengi, wamekuwa na ushirikiano na taasisi mbalimbali ambao umewezesha utekelezwaji wa mikakati na programu mbalim¬bali.
Miongoni mwa programu am¬bazo zimetokana na ushirikiano huo ni Kongamano na Soko la Wa¬nawake na Dijitali lililofanyika No¬vemba 30, 2024.
Kongamano hilo lililowafikia wanawake zaidi ya 150 liliandaliwa na LP Digital kupitia mpango wa wanawake na teknolojia, chini ya The Launchpad Tanzania lililenga kutumia ubunifu wa kidijitali kuku¬za biashara zinazoongozwa na wa¬nawake. Hafla hiyo ililenga kuziba pengo lililopo kati ya wajasiriamali wanawake na fursa za kidijitali.
Jitihada nyingine ni; ufadhili wa mafunzo kwa vijana 10 (wanawake 6 na wanaume wanne) katika kipin¬di cha miaka mitatu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Kituo cha Vija¬na cha Don Bosco Iringa, kuwafikia wasichana 500 mwaka 2023 mkoani Mara kupitia mpango wa Namthamini wa East Africa Radio na usambazaji wa taulo zinazoweza kutumika tena (Tumaini Kits) kwa wasichana 315 wa Zanzibar n.k.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu, Benki ya Diamond Trust Banki¬naanda hafla za kusherehekea ma¬fanikio ya wanawake na kuongeza uelewa kuhusu usawa wa kijinsia. “Tunashiriki katika vikao, mazung¬umzo na mikutano mbalimbali am¬bayo yanalenga kuonyesha vipaji vya wanawake na uwezo wao wana¬powezeshwa.”
Mbali na hayo benki hiyo pia inafanya miradi ya kusaidia jamii (CSR) Initiatives zinazohusisha sekta mbalimbali ikiwemo afya, ku¬toa elimu ya kifedha katika shule na vyuo mbalimbali.
Ushuhuda kutoka kwa Maryvine Peter
Meneja wa Tawi la DTB Centre wa benki hiyo, Bi. Maryvine Peter amesema ameanza safari yake ndani ya Diamond Trust Bank akiwa Karani mwaka 2014 nafsi ambayo ilimpa uzoefu wa kutoa huduma kwa wateja.
“Nilianza kazi katika BDiamond Trust Bank mwaka 2014 kama Ka¬rani, ambapo nilipata uzoefu katika kutoa huduma kwa wateja na shu¬ghuli za benki. Kwa miaka mingi, niliitumia kila fursa niliyopata ku¬jifunza, jambo ambalo lilisababi¬sha kupandishwa cheo hadi kuwa meneja wa tawi mwaka wa 2022,” anasema amesema Maryvine.
Ameendelea kuwa “Kuwa ki¬ongozi katika tawi jipya linalowa¬hudumia watu wenye kipato ki¬kubwa (HNI) ni changamoto lakini pia ni fursa ya kukuwa na kujifunza zaidi. Kama mwanzilishi wa jukumu hili, niliweza kuanzisha uhusiano na kukuza biashara katika tawi kwa ki¬asi kikubwa. Safari yangu imekuwa ikiongozwa na kujifunza, kubadilika kutokana na mazingira pamoja na kujitoa katika utoaji wa huduma bora.”
Kuhusu mafanikio yake ndani ya benki hiyo Maryvine anasema “Tan¬gu kuwa meneja wa tawi, mafanikio yangu makubwa ni kutengeneza msingi imara wa wateja wa HNI na kukuza biashara ya tawi letu huku nikiboresha viwango vya huduma ili kuhakikisha tunatoa huduma bora za kibenki kwa wateja ambayo sio tu iliongeza kuwaridhisha lakini pia imeongeza uaminifu na uhusiano bora kwa wateja wetu.”
Amesema Diamond Trust Bank imekuwa muhimu katika ukuaji wake kikazi na maendeleo ya uon¬gozi. Hii ni kwa sababu benki hiyo inatoa programu mbalimbali za mafunzo ambazo zimempa ujuzi muhimu wa kusimamia timu kwa ufanisi jambo ambalo pia lilimjen¬gea ujasiri na uwezo wa kuongoza katika mazingira ya ushindani.
Maryvine anasema “Kwa wa¬nawake vijana wanaotaka kuingia katika sekta ya benki, ushauri wan¬gu ni kuwa wastahimilivu. Wanat¬akiwa kutafuta ushauri na kujenga mtandao imara. Wasisite kutumia fursa zenye changamoto ambazo zitawasaidia kusonga mbele zaidi. Waamini katika uwezo, waweke malengo na kuyasimamia.”