Diamond alia Tanzania kukosa Arena

Zanzibar. Staa wa Bongo Flava, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameiomba Serikali kutengeneza Arena kwa ajili ya matamasha makubwa ya muziki kama Trace.

Diamond ameyasema hayo Februari 26,2025 wakati akiingia kwenye tuzo za muziki za Trace zinazofanyika Zanzibar Kisiwani Unguja.

“Imagine Arusha kunatengenezwa uwanja mwingine. Tungepata Arena na sisi ingetusaidia, hizi event zikifanyika nyingi zinatukuza. Wasanii wa Kitanzania tumejitahidi sana kuweka nguvu ya kisanaa ambayo inaonekana.

“Kwa hiyo tunaomba serikali ituunge mkono kwenye kutuwekea Arena. Na itasaidia vitu vingi, Basketball, Netball, kutafanyika mikutano na mambo mbalimbali. Sanaa ya Tanzania ni kubwa sana lakini kwa sababu tunakosa vitu kama Arena unakuta watu wanaenda kwenye nchi za watu wengine,” amesema Diamond

Aidha nyota huyo wa muziki ameongezea kwa kutolea mfano nchini Rwanda wanavyonufaika na Arena zao
 

“Mimi msanii naongea na Basata kila siku lakini sitaki kuamini kama fedha hamna ni kuamua tu naamini Dk Samia Suluhu Hassan ni mtu ambaye ameleta mageuzi, katika vitengo tofauti tofauti tunamuomba na sisi kama wasanii atutengenezee Arena,” amesema Diamond