CPJ: 2024 ndio mwaka mbaya zaidi katika historia kwa waandishi wa habari, Israel imeua idadi kubwa zaidi

Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) imesema mwaka 2024 ulikuwa mwaka mbaya zaidi katika historia iliyorekodiwa kwa waandishi wa habari waliouawa, na kwamba utawala wa Israel unawajibika kwa kuua asilimia 70 ya waandishi 124 waliopoteza maisha mwaka jana.