Cote Dvoire: Chama kikuu cha upinzani chaitisha maandamano

Nchini Cote Dvoire, chama kikuu cha upinzani PDCI kimeitisha maandamano mbele ya Mahakama hivi leo, kulaani hatua ya kuondolewa kwa mwanasiasa wake Tidjane Thiam katika orodha ya wagombea urais, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya chama hicho, inakuja baada ya siku ya Jumanne, Mahakama jijini Abidjan, kuamua kuwa Tidjane Thiam hana sifa ya kuwania urais kwa sababu alikuwa amepoteza uraia wa Cote Dvoire, wakati alipoomba kuwa raia wa Ufaransa mwaka 1987.

Uamuzi huu wa Mahakama hauwezi kupingwa na hii inamaanisha kuwa, Thiam hatakuwa miongoni mwa wagombea urais nchini humo.

Uamuzi dhidi ya Thiam ulitolewa akiwa nchini Ufaransa, ameiambia AFP kuwa licha ya uamuzi huo wa Mahakama, chama chake hakina mpango wa kuwasilisha mgombea mwingine, na kuongeza kuwa atakata rufaa kwenye Mahakama ya kikanda ya Jumuiya ya ECOWAS.

Rais wa zamani Laurent Gbagbo, naye pia amezuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo. Chama tawala hakijamtangaza mgombea wake, lakini kimekuwa kikimshiniiza rais Alassane Ouattara, mwenye umri wa miaka 83 kuwania tena kwa muhula wa nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *