
Nchini Côte d’Ivoire, vyama kumi na tano vya upinzani vinazindua muungano siku ya Jumatatu, Machi 10, kwa nia ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 25, 2025. Miongoni mwa vyama vya siasa vinavyounda muungano huo ni chama cha PDCI, chama cha Movement of Capable Generations (MGC) cha aliyekuwa mke wa rais wa zamani, Simone Ehivet-Gbagbo au chama cha Cojep cha Charles Blé Goudé. Muungano huo unaitwa Muungano wa mabadilishano ya amani – Cap Côte d’Ivoire, bila chama cha PPA-CI cha Laurent Gbagbo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Abdoul Aziz Diallo
Jukwaa hili jipya linaloitwa Muungano wa mabadilishano ya amani – Cap Côte d’Ivoire, linalenga kujima nguvu katika mchakato huu wa uchaguzi. Miongoni mwa matakwa yake makuu ni kurekebishwa kwa orodha ya wapiga kura kabla ya uchaguzi wa urais, kuchapishwa kwa kituo cha kupigia kura cha matokeo na kituo cha kupigia kura na ukaguzi wa orodha ya wapiga kura.
“Kupata mageuzi ya uchaguzi”
“Lengo ni kupigania mageuzi ya uchaguzi ambayo yanahakikisha uchaguzi wa uwazi, wa kuaminika na usio na ghasia,” anaeleza Dominique Traoré, naibu kiongozi wa muungano huu wa MGC. Lakini zaidi ya matakwa hayo, swali linazuka: je, muungano huu utafika hadi kumteua mgombea mmoja kwa uchaguzi wa urais? “Masharti ya ushiriki yatajadiliwa ndani ya jukwaa,” anajibu Soumaïla Bredoumy, msemaji wa PDCI.
Hata hivyo, kutokuwepo moja ya vyama vikuu, kile cha PPA-CI, chama cha rais wa zamani Laurent Gbagbo kunatia mashaka katika muungano huo. Kulingana na kongozi wake mtendaji, Sébastien Djédjé Dano, chama “kinafanya kazi kwa wito wa umoja wa upinzani uliozinduliwa na Laurent Gbagbo mwzei Julai mwaka uliyopita huko Bonoua.”
Pembetatu inayoweza kudhoofisha chama kilicho madarakani…
“Uthibitisho kwamba upinzani haulingani,” anachanganua mtaalamu wa masuala ya siasa Geoffroy Julien Kouao. Kwa mwanasheria huyu, usanidi huu unafungua njia ya uchaguzi wa kambi tatu: “RHDP kwa upande mmoja, PPA-CI kwa upande mwingine na muungano huu mpya unaoongozwa na PDCI-RDA.” Na anaongeza: “Kinyume na vile mtu anavyoweza kufikiria, kambi hizi tatu zinaweza kudhoofisha chama kilicho madarakani endapo kutakuwa na duru ya pili.”