Côte d’Ivoire: Mahakama yamuondoa kiongozi wa upinzani kwenye orodha ya wapiga kura

Mahakama ya Mwanzo ya Abidjan, nchini Côte d’Ivoire, siku ya Jumanne, Aprili 22, imeagiza kuondolewa kwa Tidjane Thiam kwenye orodha ya wapiga kura. Jaji anabaini kwamba hakuwa tena na uraia wa Côte d’Ivoire wakati alipojumuishwa kwenye orodha hiyo mnamo 2022.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne

Jaji ameamua kwamba Tidjane Thiam alipoteza uraia wake wa Côte d’Ivoire alipopata uraia wa Ufaransa. Inatokana na Kifungu cha 48 cha Kanuni ya Uraia ambayo inasema kwamba mtu mzima wa Côte d’Ivoire atapoteza uraia wa Côte d’Ivoire baada ya miaka 15 ikiwa atapata urai mwingine kwa hiari.

Mawakili wa Tidjane Thiam walijaribu kuthibitisha kwamba mteja wao alizaliwa Mfaransa na kwamba kwa hivyo, kifungu hiki cha Kanuni za Uraia hakitumiki kwa mteja wao kwa vile alizaliwa akiwa na urai pacha. Wanadai kuwa wamewasilisha hati za kiutawala kwa uamuzi huu. “Tunaheshimu uamuzi wa jaji, lakini hatukubaliani nao,” amesema Wakili Rodrigue Dadjé, mwanasheria wa Tidjane Thiam, ambaye alikatishwa tamaa na uamuzi wa mahakama.

Yote yalianza kwa mpiga kura ambaye, wakati wa mzozo wa orodha ya wapiga kura, aliwasiliana na Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) kuomba kuondolewa kwa Tidjane Thiam kwenye orodha hiyo, akibaini kwamba yeye sio tena raia wa Côte d’Ivoire. CEI ilitupilia mbali madai ya mwombaji, ambaye kisha akageukia Mahakama ya mwanzo. Kesi ilisikilizwa kwa faragha siku ya Jumanne asubuhi. Kikao ambacho kila upande uliwasilisha hoja zake.

Tidjane Thiam anashutumu “kunyimwa haki”

Kwa kuwa Tidjane Thiam, kwa wakati huu, hatastahili kwa uchaguzi wa urais mnamo Oktoba 25, kwa kuwa si mpiga kura. Ikumbukwe pia kwamba katika hatua hii, hakuna njia nyingine ya kuomba kusajiliwa upya kwenye orodha ya wapiga kura. “Sikubali kunyimwa haki yangu: sio haki, sio haki na haieleweki,” Tidjane Thiam alisisitiza katika video iliyorushwa kwenye mtandao wa kijamii. Tidjane Thiam alishutumu “kunyimwa haki” na kutoa wito wa mazungumzo ya kutatua hali hiyo: “Tunahimiza pande zote kushiriki katika mazungumzo ya kujenga ili kura ya mwezi Oktoba iafiki viwango vya kimataifa na kwamba hakuna mtu yeyote anayetengwa katika mchakato wa uchaguzi,” imeandikwa taarifa iliyotolewa Jumanne jioni.

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, Tidjane Thiam alisema kuwa “serikali ndiyo kwanza imemuondoa mpinzani wake mkubwa kupitia hoja za kisheria zisizo za haki na zisizoeleweka […] Hili si jambo la kawaida na si taswira ambayo nataka nchi yetu iwe nayo.”

Aliongeza kuwa “PDCI imeungana nyuma yangu. Hakutakuwa na mpango wa pili, hakuna mpango wa tatu. Tunataka kwenda kwenye uchaguzi huu tukiwakilishwa na mgombea ambaye PDCI ilimchagua kwa uhuru kwa 99.5% wakati huo, na kwa uwazi kabisa na kwa njia ya kidemokrasia.” “Tuwe na hakika kwamba nitadhamiria kuwa mgombea urais wa Jamhuri,” alisema katika kuhitimisha taarifa yake.

Lakini kwa sasa, Tidjane Thiam atatetea kesi yake tena siku ya Alhamisi, mbele ya Mahakama ya Mwanzo ya Abidjan.

Jaji lazima sasa aarifu CEI kuhusu uamuzi wake. Orodha ya mwisho ya wapiga kura itachapishwa mnamo Juni 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *