Congo-Brazzaville: Azimio la Umoja wa Mataifa la kuimarisha ulinzi wa mimea duniani

Kwa nia ya kuimarisha uoto wa kimataifa na kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya hali ya hewa, Umoja wa Mataifa ulipitisha, Aprili 16, kufuatia pendekezo kutoka Congo-Brazzaville, azimio kuhusu muongo wa kimataifa wa upandaji miti na kukuza misitu Habari hizo zimethibitishwa siku ya Alhamisi, Aprili 24, na serikali ya Kongo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Brazzaville, Loïcia Martial

Mpango huo unalenga kuongeza eneo la mimea duniani kwa asilimia 4 kati ya mwaka 2027 na 2036. Mkakati wa kufikia lengo hili unaandaliwa hivi sasa. Rosalie Matondo ni Waziri wa Uchumi wa Misitu wa Kongo: “Ni wakati wa kuchukua njia mbadala ya kuunda misitu ya bandia, ili tuweze kubadili mwelekeo huu kuelekea ukataji miti na uharibifu wa mazingira.”

Upandaji miti

“Lakini tunataka, katika muongo huo ambao tumependekeza kwa ulimwengu, kuongeza maeneo ya misitu kupitia upandaji miti,” ameongeza. Upandaji miti ni upandaji wa miti katika maeneo yasiyo na misitu. Mpango huo unapanga, kwa mfano, kustawisha maeneo ya savana duniani kote.

Maixent Animba Emeka wa shirika la kiraia anakaribisha mradi huo, lakini anasahihisha kauli yake: “Hii isitufanye tusahau ukweli kwamba hatupaswi kuharibu au kusababisha kupotea kwa mifumo mingine ya ikolojia kama savana, kwa sababu ya misitu, kwa sababu savana pia ni makazi ya baadhi ya wanyama,” amesema. Dunia inapoteza hekta milioni kumi za misitu kila mwaka kutokana na ukataji miti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *