Christophe Lutundula: Makubaliano ya M23 na Serikali mpaka Kagame aidhinishe

Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kigeni ya Baraza la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Christophe Lutundula amesema kuchanganya mchakato wa Luanda na ule wa Nairobi kwa ajili ya kusaka amani sio jambo jema, sababu moja ni nyongeza ya mwingine.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Ni michakato miwili tofauti, na ikichanganywa, madhara yake ni ambayo ni mabaya sana, ni kuidhinisha madai ya rais Paul Kagame ambaye amekuwa akisema kwamba matatizo ya Congo ni ya wa Congo wao kwa wao na hapo utakuwa umemuondoa.

Na pili kama hatujafikia makubaliano na M23, jeshi la Rwanda litalazimika kuendelea kusalia nchini DRC wakati tunafahamu kwamba  maelewano na M23 yanaweza kupita tu ikiwa Rais Kagame ataidhinisha, ikiwa tu atapewa nafasi ya kuendelea kuwa na nafasi ya unyonyaji wa kiuchumi na kuwa na ushawishi, haya ni madhara ambayo hatupashwi kupuuzia.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi walikutana na Emiri wa Qatar, Tamim ben Hamad al-Thani, Doha Tarehe 18 Machi 2025.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi walikutana na Emiri wa Qatar, Tamim ben Hamad al-Thani, Doha Tarehe 18 Machi 2025. via REUTERS – Qatar’s Ministry of Foreign Affa

Akiulizwa kuhusu iwapo anaunga mkono majadiliano ya moja kwa moja baina ya serikali na M23, kiongozi huyo amesema hilo sio tatizo, sababu ukianzisha mchakato wa kumdhihaki rais Tshisekedi, kuwadhihaki wananchi wa Congo hilo hawezi kukubali, aidha serikali inarejeshaje maeneo yaliokaliwa na M23 bila majadiliano?

Christophe Lutundula amesema M23 haipo, ni jeshi la Rwanda, ni ukweli ambao hauhitaji mjadala tena, Rwanda iondoke Congo, sababu wanatwambia ni matatizo ya wa congo wenyewe kwa wenyewe sasa watuache tutatuwe matatizo yetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *