Chino kurudi shule, amtaja mzungu

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Chino Kidd amesema pamoja na umaarufu wake anahitaji sana kurudi shule ili aongeze uwezo wake wa kuimba.

Chino ambaye anapendelea kuimba mtindo wa Amapiano, amesema anaamini baada ya kutimiza ndoto yake ya kurudi shule, mambo mengi yatakuwa mazuri kwani hata muziki wake utazidi kufika kimataifa ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo ambazo zinaweza kuinua uchumi wa Taifa.

CHINO Pict

“Mimi shule lazima nirudi tu,  kwani kule ndo kwenye mipango na maisha mazuri, naelewa bila shule mambo mengi tunakuwa tunafanya lakini tunakosea, mashabiki wangu ambao wanatamani kuniona nikirudi shule wanaamini nitafanya hivyo kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kazi yangu,” amesema Chino.

Amesema pia kwa sasa ameanza kujua lugha ya Kiingereza kidogo na ujuzi huo amepata kwa mpenzi wake mzungu.

“Sasa hivi nimeshaanza kuifahamu lugha ya Kiingereza, natamani sana kuifahamu kuongea zaidi, mpenzi wangu mzungu anajitihida kubwa sana kunifundisha, japo watu wameanza kuzusha nimeachana nae. Mimi ni mwehu niachane na mwalimu wangu wa lugha? bado nipo naye na ninatamba naye,” aeisema Chino.

Ikumbukwe Chino alikuwa dansa  kabla ya kuingia kwenye kuimba. Katika moja ya mahojiano yake na Mwananchi aliwahi kusema hakuwahi kujifunza uchezaji wake mahali, bali ni vaibu tu ilitokea, akajikuta anapenda kucheza na mwili unampa ushirikiano.

Aidha jina la Chino Wana Man, lilitokana na kupenda namna kabila la Wasukuma wanavyoitana mwanawane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *