China yaituhumu Marekani kuwa na sera za nyuso mbili

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeutuhumu utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kufuata sera za ” nyuso mbili” na kuahidi “kukabiliana kwa uthabiti” na mashinikizo yanayoongezeka ya vikwazo, huku mvutano kati ya nchi hizo mbili zenye nguvu za kiuchumi ukiendelea kutokota.