
China siku ya Alhamisi imeitaka Marekani kufuta mara moja ushuru wake wa hivi karibuni na kuahidi hatua za kukabiliana nazo ili kulinda maslahi yake, baada ya Rais Donald Trump kutangaza kutoza ushuru mkubwa kwa washirika wote wa kibiashara wa Marekani duniani kote.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi huo wa Marekani unapuuza uwiano wa maslahi yaliyofikiwa katika mazungumzo ya biashara ya pande nyingi kwa miaka mingi na ukweli kwamba China imenufaika kwa muda mrefu kutokana na biashara ya kimataifa, imesema taarifa ya Wizara ya Biashara ya China.
“China inapinga kithabiti hili na itachukua hatua za kujiubu hatua hizo kwa kulinda haki na maslahi yake,” wizara hiyo imesema, huku mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi duniani yakionekana kuzama katika vita vya kibiashara vinavyotishia kuvuruga minyororo ya ugavi duniani.
Siku ya Jumatano, Bw.Trump alitangaza kuwa China itapigwa ushuru wa asilimia 34, juu ya asilimia 20 iliyoweka mapema mwaka huu, na kufikisha jumla ya ushuru mpya hadi asilimia 54 na kukaribia asilimia 60 ambayo alitishia kuweka wakati wa kampeni yake ya uchaguzi.
Wauzaji bidhaa nje wa China, kama wale walio katika uchumi mwingine wote, watakabiliwa na ushuru wa kimsingi wa asilimia 10, kama sehemu ya ushuru mpya wa asilimia 34, kwa karibu bidhaa zote zinazosafirishwa hadi kwenye uchumi mkubwa zaidi wa watumiaji duniani kuanzia Jumamosi, kabla ya “ushuru wa kulipiza” uliobaki kuanza kutekelezwa kuanzia Aprili 9.
Bw. Trump pia ametia saini agizo lililolenga kuziba mwanya wa biashara unaojulikana kama “de minimis,” ambao umeruhusu vifurushi vya bei ya chini kutoka China na Hong Kong kuingia Marekani bila ushuru wa forodha.
REUTERS