China yaiambia G20: Lazima dunia iisikilize Afrika, iyape uzito masuala yanayoitia wasiwasi

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema, lazima dunia isikilize “kile Afrika inachosema” na kuuchukulia wasiwasi ilionao Afrika “kwa uzito”. Wang ameyasema hayo katika hotuba yake mbele ya hadhara ya washiriki wa mkutano wa Kundi la Mataifa 20 (G20) unaofanyika mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.