Chelsea yasajili wawili kwa mpigo

London, England. Klabu ya Chelsea imefanikiwa kufanya usajili wa mastaa wawili kwa mpigo kutoka kwenye kikosi cha  Sporting Lisbon ya Ureno.

Chelsea imetumia kitita cha pauni 62.4 milioni (sawa na shilingi bilioni 212) kwa ajili ya kuwasajili makinda Geovany Quenda na Dario Essugo ambao wameonyesha kiwango bora kwenye michezo kadhaa waliocheza.

Klabu hiyo ya Ureno imeshatoa taarifa kuwa usajili wa wachezaji hao umefanikiwa na wataanza mmoja ataanza kuitumikia klabu hiyo ya London kuanzia mwanzoni mwa msimu ujao.

Inaelezwa kuwa Quenda ameigharimu timu hiyo kitita cha pauni 43.7 milioni, huku Essugo yeye akijiunga na Chelsea kwa kitita cha pauni 18.7 milioni.

Dili la Quenda pamoja na kwamba limekamilika lakini staa huyo ambaye anaichezea timu ya Taifa ya Ureno chini ya miaka 21, atajiunga na Chelsea kwenye majira ya joto mwaka 2026.

Hili ni pigo kwa Man United ambao walikuwa wanaamini kuwa wanaweza kumsajili Quenda, ambaye mwishoni mwa msimu huu atakuwa amefikisha miaka 18 na aliwahi kucheza chini ya kocha wa sasa wa United Ruben Amorim akiwa na Sporting.

Amorim ndiye alimpandisha Quenda na kuwa mchezaji pekee kutoka kwenye timu ya vijana kuichezea Sporting akiwa na umri wa miaka 16.

“Huyu ni mchezaji mzuri mwenye kiwango bora sana, anafahamu jinsi ambavyo soka linataka na ana uwezo mzuri sana,” aliwahi kusema Amorim.

Pamoja kwamba amezaliwa Guinea-Bissau, Quenda aliamua kuitumikia Ureno, akiwa ameshacheza kwenye timu za vijana chini ya miaka 17 na 21, kwa msimu huu amefanikiwa kucheza michezo 44 akifunga mabao mawili na kutoa pasi nane za mabao.

Kwa upande wa Essugo, ambaye yupo kwenye kikosi cha Ureno chini ya miaka 21 kwa sasa anacheza kwa mkopo kwenye kikosi cha Las Palmas cha Brazil akiwa amecheza michezo 17 na kufunga bao moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *