
Marekani. Zana ya kidijitali ya Akili Mnemba (AI), ChatGPT imeongoza kwa kutumiwa zaidi Januari 2025 ikilinganishwa na zana zingine.
Kwa mujibu wa takwimu za tovuti Visual Capitalist ChatGPT ilitembelewa mara bilioni 4.7 Januari 2025 ikifuatiwa na Canva iliyotembelewa mara milioni 887.
Google translate ilishika nafasi ya tatu kwa kutembelewa mara milioni 595, DeepSeek ikitembelewa mara milioni 268 na nafasi ya tano ikishika Character.AI iliyotembelewa mara milioni 226 Januari 2025.
Hii hapa orodha yake:
1. ChatGPT: Bilioni 4.7
2. Canva : Milioni 887
3. Google Translate: Milioni 595
4. DeepSeek: Milioni 268
5. Character.AI: Milioni 226
Ukuaji huu wa ChatGPT unaonyesha jinsi teknolojia ya mazungumzo ya AI inavyozidi kupenya katika shughuli mbalimbali, ikiwemo huduma za wateja, elimu, na utafiti.
Tovuti ya Visual Capitalist imeripoti kuwa; “Wataalamu wanasema mwelekeo huu unaashiria kuendelea kukua kwa matumizi ya mifumo ya kujifunza kwa kina (deep learning) na AI katika nyanja nyingi, huku watumiaji wakivutiwa na uwezo wa zana hizi kurahisisha kazi za kila siku.”
Kwa mujibu wa Tovuti ya takwimu ya Visual Capitalist imeandika kuwa: “Ongezeko la matumizi ya ChatGPT na zana nyingine za AI linadhihirisha mapinduzi katika teknolojia ya mawasiliano na ubunifu, na ni wazi kwamba mashindano ya kuwa zana bora za kisasa katika nyanja mbalimbali za kiteknolojia yanazidi kushika kasi.”