Charles Hilary kuzikwa Zanzibar Mei 14, hii hapa ratiba kamili

Unguja. Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) unatarajiwa kuzikwa Jumatano Mei 14, 2025 katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.

Katika ratiba ya serikali iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, mwili wa marehemu utatolewa katika hospitali ya Mloganzila na kupelekwa nyumbani kwake Kibamba CCM kesho Mei 12, 2025 saa 11:00 jioni kwa ajili ya maombelezo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mwili utaondoka nyumbani kwake Mei 13, 2025 saa 3:00 asubuhi na kupelekwa kanisa la Mt. Batholomayo Anglikana Ubungo kwa ibada maalumu ya kuagwa na ndugu jamaa na marafiki, kisha saa 10:00 jioni, utasafirishwa kuelekea Zanzibar.

Mwili wa marehemu utapokewa Bandarini saa 12: jioni na kupelekwa nyumbani kwao Makadara, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar na saa 1: 00 usiku zitakuwa sala na nyimbo za maombolezo.

Jumatano Aprili 14, 2025 kati ya saa 4 hadi 5:30 aubuhi mwili wa marehemu utatolewa nyumbani kupelekwa ukumbi wa zamani wa Baraza la wawakilishi, Idris-Abdulwakil.

Kuanzia saa 6 hadi 8:30 mchana, mwili wa marehemu utaagwa na viongozi wa Serikali, mabalozi, vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama, wanahabari na waombolezaji wote kwa ujumla kisha msafara utaelekea katika makaburi ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya maziko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *