Chama cha Shas chatishia kuiangusha serikali ya Netanyahu

Muungano wa Netanyahu ulio na watendaji wengi wa mrengo mkali wa kulia katika historia ya Israel, upo katika hatari wa kuporomoka kutokana na mswada ambao unaweza kubatilisha kinga iliyokuwepo ya muda mrefu kwa wayahudi wa Orthodox kutoshiriki katika shughuli za kijeshi.

Kinga hiyo inapingwa wakati Israel ikiendeleza vita vyake dhidi ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Netanyahu anapitia shinikizo kubwa kutoka kwa chama chake cha Likud, kuwajumuisha wanaume wa kiyahudi wa Orthodox kuingia jeshini na kuwaadhibu wote watakaokwepa hilo, jambo ambalo chama cha Shas inakipinga vikali.

Israel yazuia boti iliyobeba wanaharakati kuingia Gaza

Chama hicho kupitia msemaji wake Asher Medina kimemtaka Netanyahu kuweka sheria ya kuwaondoa kabisa wafuasi wake kwenye utumishi wa kijeshi na kuumpa Netanyahu siku mbili ya kutafuta suluhisho.

Serikali ya muungano Israel iliyoundwa mwaka 2022, inakijumuisha chama cha Likud, mirengo ya kulia na chama cha wayahudi wa orthodox, na kuondoka kwa chama hicho cha Shas cha kiyahudi kinaondoa uhalali wa muungano huo kuendelea kuongoza.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *