Chama cha Ben-Gvir chajitoa kwenye serikali ya Israel kupinga makubaliano ya usitishaji vita Ghaza

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Nguvu za Kiyahudi (Otzma Yehudit) cha waziri wa usalama wa ndani Itamar Ben-Gvir kimejiondoa kwenye serikali ya muungano ya utawala wa Kizayuni kulalamikia makubaliano ya kusitishwa vita katika Ukanda wa Ghaza.