Chad: Viza za Marekani zasitishwa kutolewa kwa siku 90

“Hakuna miadi ya visa inayoweza kufanywa katika Ubalozi wa Marekani huko Ndjamena.” Huu ndio ujumbe unaoonyeshwa sasa kwenye tovuti ya uwakilishi wa kidiplomasia wa Marekani nchini Chad. Tangu Machi 25, Marekani imesitisha utoaji wa viza kwa raia wa Chad kwa muda wa siku 90. Hayo yametangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Machi 27. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Ndjamena, Nadia Ben Mahfoudh

Kusitiishwa huku kwa muda kunahusu visa vya utalii, wanafunzi na biashara lakini haiwahusu waombaji wa visa vya kidiplomasia au wale walio na kadi ya kuishi nchini. Wananchi wa Chad wanaweza, hata hivyo, kutuma maombi ya visa kutoka kwa ubalozi wa Marekani katika nchi ya tatu.

“Ufafanuzi” 

Katika taarifa rasmi, Ibrahim Adam Mahamat, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad, amesema “anasikitishwa na uamuzi huu” na kuthibitisha nia yake ya kufanya kazi na mamlaka ya Marekani ili “kufafanua sababu” za kusitishwa kwa utoaji visa vya Marekai ili uamuzi huo uweze kuondolewa haraka.

Tangu Donald Trump arejee Ikulu ya Marekani, nchi nyingine zimeathiriwa na mabadiliko haya ya sheria za kuingia Marekani. Takriban siku kumi zilizopita, orodha ilivuja ikionyesha kutekelezwa kwa vikwazo vya kuingia Marekani kwa raia wa nchi 43, yakiwemo mataifa 22 ya Afrika. Nchi hizi zimegawanywa katika makundi matatu kulingana na vikwazo vilivyowekwa. Chad iko kwenye orodha ya manjano, yenye vikwazo vidogo zaidi kati ya makundi hayo matatu.

Hakuna uthibitisho rasmi 

Mataifa yaliyotajwa yatakuwa na siku sitini kurekebisha kile Washington inachokiona kuwa kushindwa kwa usalama. Kwa wakati huu, habari hii bado haijathibitishwa rasmi na serikali ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *