
Kiongozi wa upinzani nchini Chad Succès Masra amehojiwa na maafisa wa Mahakama siku ya Jumanne, Mei 20, 2025, siku nzima. Anatazamiwa kufika mbele ya mwendesha mashtaka leo Jumatano Mei 21, ambaye ataamua ikiwa rais wa chama cha Transfomateurs atashtakiwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu huko N’Djamena, Victor Mauriat
Succès Masra alianza kusikilizwa saa 3 asubuhi ya Jumanne katika ofisi za mahakama, ambapo alihojiwa siku nzima na Mkurugenzi wa Taasisi na wapelelezi. Waziri mkuu huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kurusha sauti kwenye mitandao ya kijamii ambayo, kulingana na mwendesha mashtaka na serikali ya Chad, ilichochea chuki dhidi ya watu wanaohamahama kusini mwa nchi hiyo.
Timu ya utetezi ya Succès Masra inaeleza kuwa huu ni wito wa kujilinda na sio kuwashambulia watu wasio na hatia. Na juu ya yote, ilitangazwa Mei 2023, miaka miwili kabla ya mauaji ya Mandakao, katika muktadha wa vurugu kati ya jamii. Kulingana na mawakili wake, hili ndilo suala ambalo kesi ya Jumanne iliangazia. Wanabaini kwamba majadiliano “yalikwenda vizuri” na wana matumaini juu ya uamuzi wa mwendesha mashtaka, ambaye ataamua baadaye leo ikiwa atandeleza au la kesi dhidi ya kiongozi wa chama cha Transformateurs.