Chad: Muda wa kuzuiliwa kwa mwanahabari wetu Olivier Monodji uwarefushwa hadi Jumatatu Machi 10

Kufuatia mahojiano mapya katika majengo ya kitengo cha mahakama kinachojihusisha na uchunguzi siku ya Jumamosi, Machi 8, muda wa kuzuiliwa kwa Olivier Monodjime umeongeza hadi Jumatatu, atakapofikishwa mbele ya mwendesha mashtaka wa umma wa Ndjamena. Ingawa kesi hiyo ilifanyika katika mazingira mazuri safari hii, bado mwenzetu hajafahamishwa sababu za kukamatwa kwake.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Alipokamatwa siku ya Jumatano Machi 5 huko Ndjamena bila kufahamishwa sababu za kukamatwa kwake, Olivier Monodji hatatoka katika chumba chake kabla ya Jumatatu Machi 10. Baada ya kuhojiwa kwa saa nne siku ya Jumamosi na maafisa watatu wa kitengo cha mahakama kinachojihusisha na uchunguzi, mkurugenzi wa uchapishaji wa Gazeti la Le Pays – ambaye pia ni mwanahabari wa RFI nchini Chad – alifahamu kuhusu kuongezwa kwa muda wa kifungo chake, uamuzi ambao wakili wake anaelezea maskitiko yake huku akisubiri kujua sababu za kukamatwa kwa mwenzetu. “Polisi wa mahakama hawakuweza kutueleza mteja wangu anatuhumiwa kwa kosa gani. Kwa hivyo tunasubiri Jumatatu ili kujua. Ni jamo la kusikitisha kuona waandishi wa habari bado wanakamatwa katika karne ya 21: kweli ni kutoka enzi nyingine! “, wakili Allatha Amos amesema.

“Kuachiliwa bila masharti”

Siku ya Jumatatu Machi 10, Olivier Monodji atafikishwa mbele ya mwendesha mashtaka wa umma wa mahakama kuu ya Ndjamena. “Kuanzia sasa na kuendelea, ni yeye pekee anayeweza kutueleza kwa nini anazuiliwa katika majengo ya polisi wakati ametoa dhamana ya kutosha ya uwakilishi,” anasema wakili Allatha Amos, ambaye hata hivyo anakiri kwamba mahojiano ya Jumamosi, Machi 8, yalifanyika katika mazingira mazuri kuliko yale ya siku iliyopita. “Tofauti na jana [Ijumaa] tulipolazimika kukumbusha kanuni za utaratibu, leo mambo yamefanyika kwa mujibu wa haki ya utetezi,” ameeleza tena kabla ya kwa mara nyingine kutaka “kuachiliwa bila masharti” kwa Olivier Monodji kwa vile bado hajui kwa nini anazuiliwa.

Kutokana na kitendo ambacho kinaelezea kama “kukamatwa kiholela”, chama cha Waandishi wa Habari wa Chad (UJT) kwa upande wake, kimeelezea wasiwasi wake mkubwa. Pia kinalaani shambulizi kubwa dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari na dhamana ya mahakama iliyotolewa katika Katiba ya Chad na kwa hiyo pia kinataka kuachiliwa mara moja kwa Olivier Monodji na kurejeshwa kwa vifaa vyake vya kazi.