
Nchini Chad, kesi za kisheria zinazomhusu Succès Masra zilianza Jumatatu, Mei 19, 2025, lakini kwa fujo. Waziri Mkuu wa zamani na rais wa chama cha Transformateurs, akiwa chini ya ulinzi wa polisi tangu Ijumaa asubuhi, anashutumiwa hasa kwa kuchochea chuki na kusababisha mauaji ya wafugaji 42 kitendo kilichotekelezwa na wakulima katika eneo lake la asili wiki iliyopita. Alitakiwa kuhojiwa na wachunguzi siku ya Jumatatu asubuhi, lakini mawakili wake walieleza kuwa hawakuweza kuhudhuria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu huko Ndjamena, Victor Mauriat
Mawakili wa Succès Masra wameeleza jioni ya jana kwamba walirudishwa nyuma walipofika mbele mlango wa kuingia katika Ofisi ya Uratibu wa Polisi wa Mahakama, ambapo mteja wao alikuwa akihojiwa na wachunguzi.
Kulingana na mawakili wake, afisa mmoja aliwatishia na kuwatusi. “Majambazi, thubutuni kuingia kama nyinyi ni wanaume,” inasemekana aliwaambia. Wakati huo huo, ndani Ofisi ya Uratibu wa Polisi, kiongozi wa chama cha Transfomateurs alikataa kujibu maswali kutoka kwa maafisa wa polisi wa mahakama kwa kukosekana kwa mawakili wake.
Malalamiko yaliwasilishwa kwa matusi na vitisho vya umma, wameeleza wawakilishi wa Succès Masra, ambao hata hivyo wamesema kwamba wakalaafisa huyo aliadhibiwa na wakubwa wake. Lakini kutokana na kile wanachoeleza kuwa ni “tukio kubwa,” mawakili hao wameomba kesi hiyo ya kumsikiliza mteja wao iahirishe hadi leo Jumanne asubuhi.
Kwa upande wa chama, walihojia jana jioni, “inabakia kuonekana ikiwa tukio hili lilikusudiwa kuwazuia mawakili kuhudhuria kusikilizwa kwa mteja wao.” Hatimaye, mamlaka haikutaka kutoa maoni yoyote juu ya kesi hiyo, msemaji wa serikali amesema kwamba “walirejelea mfumo wa haki katika kesi inayomhusu mshtakiwa kama nyingine yoyote.”
Kesi za kisheria zinatarajiwa kuanza leo Jumanne. Kiongozi wa chama cha Transfomateurs atalazimika kutoa ushahidi wa rekodi ya sauti iliyorekodiwa Mei 2023 ambapo anatoa wito wa kujilinda kwa Wakristo kusini mwa nchi. Wito ambao mamlaka sasa wanauelezea kama “uchochezi wa chuki” na lawama kwa vurugu za wiki iliyopita kati ya makabila mawili.