Chad: Bunge la Seneti la kwanza katika Historia ya nchi lamchagua Haroun Kabadi kama rais

Nchini Chad, Bunge la Seneti la kwanza katika historia ya nchi hiyo limemchagua rais wake siku ya Ijumaa, Machi 7, 2025: Haroun Kabadi ameteuliwa kwa shangwe za maseneta 69 waliochaguliwa hivi karibuni au kuteuliwa na Rais Mahamat Idriss Déby. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Ndjamena, Nadia Ben Mahfoudh

Mtu ambaye daima amekuwa mwaminifu kwa familia ya Déby na kwa Patriotic Salvation Movement (MPS), chama kilichkuwa madarakani kwa miongo mitatu, hivyo anakuwa kiongozi wa pili muhimu zaidi nchini: kwa mujibu wa Katiba, kwa hakika ni Rais wa Bunge la Seneti anakaimu nafasi ya rais wa Jamhuri endapo itatokea ombwe la uongozi wa nchi.

“Uzoefu mzuri”

Haroun Kabadi ni “mtu mwenye uzoefu mkubwa ambaye amejua siri zote za siasa na mamlaka,” anabaini Djimtibaye Lapia, mkuu wake wa zamani katika ofisi ya rais. Rais wa Bunge la taifa na kisha rais wa Baraza la taifa la Mpito tangu kifo cha Idriss Déby, Waziri Mkuu na mara kadhaa waziri au mshauri wa urais, Haroun Kabadi ameshikilia nyadhifa nyingi za juu za kisiasa katika miaka thelathini iliyopita.

Chari ya Kati

Haroun Kabadi ambaye anatoka jimbo la Moyen-Chari kusini mwa Chad, pia anajulikana kama mtu aliyepitisha azimio la kuwainua Mahamat Idriss Déby na baba yake hadi cheo cha marshal. Kufuatia kifo cha Idriss Déby, Haroun Kabadi, rais wa wakati huo wa Bunge la taifa, aliachana na mipango yake ya kuchukua madaraka, hivyo kutoa nafasi kwa kipindi cha mpito kinachoongozwa na rais wa sasa wa Chad.