
Msanii anayefanya vizuri kwenye Bongo Movie na ambaye pia ni video vixen, Caren Simba amefunguka madai ya kuhusishwa kimapenzi na nyota wa Yanga, Pacome Zouzoua na kuweka wazi ukaribu wao ni kwa sababu kila mmoja ni shabiki wa mwenzake katika kazi zao.
Caren alisema kinachomponza hadi kukutana na uvumi wa kutoka kimapenzi na Pacome ni kupenda soka na kwa sababu pia anaishabikia timu hiyo.
“Skendo ambayo naichukia ni hii ya kuambiwa natoka kimapenzi na Pacome, jamani mimi ni shabiki wake na yeye ni shabiki wangu katika kazi yangu ya sanaa, hivyo nakuwa naye karibu sababu ya kuzoeana na kupenda soka na sio kimapenzi, pia akiwa na nafasi ananitoa sehemu, kama kwenye muziki au sherehe yoyote.Sasa mtu kama anaonyesha mapenzi ya hivi kwa nini nisiwe naye karibu?”
“Kwanza ngoja nikwambie, sio tu Pacome kuwa naye karibu, mimi karibia wachezaji wote wa Yanga nipo nao karibu, kwa nini waseme Pacome? Nieleweke jamani, Pacome sio mpenzi wangu,” alisema Caren.
Aidha, alisema hata mchezaji wa Yanga, Khalid Aucho hana uhusiano naye zaidi ya urafiki tu.
“Jamani hawa watu mnaonipa wana wapenzi wao, sasa kwa nini mimi nahusishwa? Sasa kama Aucho naye nahusishwa naye kisa tu amenipa zawadi ya jezi, ina maana mimi sipaswi kupewa zawadi na mtu? Tena Aucho ni mshkaji sana na tunaheshimiana sana, wala sio mpenzi wangu, nawezaje kuwa na wapenzi wote hao wa timu moja, huku si kujiaibisha?”