
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inasema inataka kufungua mazungumzo ya kisiasa na upinzani miezi michache kabla ya uchaguzi wa urais mwezi Desemba mwaka huu. Taarifa zilizothibitishwa kwa RFI na Fidèle Gouandjika, mshauri wa karibu wa rais Faustin-Archange Touadéra. Ingawa Rais Faustin-Archange Touadéra anasema kwa sasa anaangazia masuala ya nchi, ugombeaji wake wa kuchaguliwa tena hauonekani kuwa wa shaka. Hiki ndicho upinzani unakataa, na umetangaza kuandaa maandamano mapya.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra alitangaza hili kwa maneneo machache Machi 30. Katika hotuba aliyoitoa wakati wa kuadhimisha miaka minne ya muhula wake wa pili, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alitangaza kwamba “anaungana na kambi ya Jamhuri kutetea katiba” ili “kuimarisha amani kwa njia ya mazungumzo.”
Kwa mujibu wa mshauri maalum wa Mkuu wa Nchi, Fidèle Gouandjika, wajumbe wa serikali, pamoja na “taasisi nyingine za jamhuri” watawajibika kuendesha mazungumzo haya. Lakini “tunasubiri BRDC itoe hoja wanazotaka kushughulikia ili serikali iweze kuanza kazi,” Fidèle Gouandjika ametuambia.
Ishara ya utulivu
Upinzani unapinga vikali muhula wa tatu unaowezekana wa Faustin-Archange Touadéra. Mnamo Machi 26, rais alimpinga waziri wake wa mambo ya ndani, na kumwamuru aidhinishe maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanyika Aprili 4. Maandamano ambayo waziri huyo alikuwa amepiga marufuku siku moja kabla.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Aprili 17, mratibu wa BRDC Crépin Mboli Goumba, ambaye alionyesha uwazi kwa wazo la mazungumzo, alishutumu “msimamo wa vyombo vya habari vilivyopangwa kudanganya,” akisema kwamba mkuu wa nchi “analazimika kutoa uhakikisho kwa jumuiya ya kimataifa.” “Tuko tayari kukutana na rais Touadéra wakati wowote wa siku au wiki ili kuweka ratiba iliyo wazi na sahihi ya mazungumzo tunayotaka,” mwanasheria huyo alisisitiza. “Kupitia dhana yetu ya BRDC na dhana yao, daima kuna nafasi ya sauti ya kati ili tuweze kusonga mbele.” » Wakati huo huo, uongozi wa BRDC umetangaza kuandaa maandamano mapya Mei 31.