
Mkurugenzi wa Gazeti la Quotidien de Bangui ambaye alikamakamatwa wiki iliyopita, aliwekwa chini ya ulinzi na kuhamishwa siku ya Jumatano, Mei 14, hadi kituo cha Ngaragba. Akishutumiwa kwa kuchochea chuki, kutoa wito wa kukaidi na kuanzisha uasi dhidi ya Katiba na mamlaka ya Serikali, Landry Nguéma Ngokpélé anakanusha shutuma hizo. Wanahabari wanaodai kuachiliwa kwa mwenzao, walisusia Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyoadhimishwa siku hiyo nchini Jamhuri ya afrika ya Kati.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu huko Bangui, Rolf Steve Domia-leu
Kesi hii inajiri wakati Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliadhimishwa siku ya Jumatano mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Tukio hilo lililopangwa kufanyika baadaye, lilisusiwa sana na waandishi wa habari wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakipinga kufungwa kwa mwenzao, tukio lililotokea siku hiyo hiyo.
“Kazi ya mwandishi wa habari inadhibitiwa kisheria. Katika tukio la kosa la vyombo vya habari, mwandishi wa habari lazima ajulishwe juu ya amri ya wito iliyotiwa saini na mkuu wa mahakama.” Amri hii inajumuisha nyaraka zote zinazojumuisha ushahidi wa kosa analodaiwa kutenda, ikiwa ni pamoja na malalamiko,” anaeleza Cyrus Sandy, mkurugenzi wa Gazeti la Média+. Ni mmoja wa wale waliokataa kushiriki katika hafla hiyo kwa sababu, kulingana na yeye, mwenzake hakuwa na haki ya utaratibu huu wa kujulishwa kosa lake. “Alichukuliwa hivyo mchana kweupe. Ni njia ya kunyamazisha vyombo vya habari. “
“Acheni mahakama ifanye kazi yake”
Baadhi ya waandishi wa habari, hata hivyo, wamechagua kuhudhuria hafla hiyo ili kuelezea wasiwasi wao kuhusu mazingira yao ya kazi. “Hii ni fursa ya kuzungumzia mazingira yetu ya kazi na matatizo yanayohusiana na kupata habari. Kwa miaka kadhaa, vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati viko mitaani kwa sababu hatuna kituo cha waandishi wa habari. “Tuko hapa pia kupendekeza kwa serikali kwamba iheshimu uhuru wa vyombo vya habari,” anaeleza Pascal Isidore Boutene, mkurugenzi wa Fair-Play.
Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali, Maxime Balalou, amejizuia kutoa maoni yoyote kuhusiana na suala hilo:
“Achani mahakama ifanye kazi yake. Sote tutajua, kwa uwazi, nini kilifanyika, kile ambacho mwenzenu anatuhumiwa.”
Akiwa amefungwa katika kituo cha Ngaragba, Landry Nguéma Ngokpélé atafikishwa mbele ya majaji siku ya Jumatatu ya wiki ijayo kwa mahojiano yake ya kwanza.