Cape Town ni mwenyeji wa mkutano wa nane wa Umoja wa Ulaya-Afrika Kusini

Mkutano huo ambao utaongozwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, pamoja na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, unatarajiwa kuangazia kuimarika kwa ushirikiano kati ya Brussels na Pretoria katika muktadha wa mivutano mikubwa ya kimataifa, haswa na Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Valentin Hugues

Mji wa Afrika Kusini wa Cape Town ni mwenyeji wa mkutano wa nane wa Umoja wa Ulaya (EU) na Afrika Kusini leo Alhamisi Machi 13, huku mvutano wa kimataifa ukiendelea kuongezeka. Muktadha – na mkutano wa kilele – ambao, kwa mujibu wa Taasisi ya Kiafrika ya Mafunzo ya Usalama (ISS), unaipa Ulaya fursa ya kujiweka kama “kinyume na matarajio ya China na ulinzi wa Marekani” katika bara la Afrika, na hasa Afrika Kusini.

Haishangazi, kwa vile Pretoria tayari ni mmoja wa washirika wakuu wa EU, kwa hiyo mkutano huo utalenga hasa kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya kami hizi mbili, wakati ambapo Marekani inazidi kuipa kisogo Afrika kwa ujumla na hasa Taifa la Upinde wa mvua (Afrika Kusini). Lengo hili pia litapatikana katika sekta ya nishati, kwa kuwa suala la kuimarisha ushirikiano kwa ajili ya mpito wa haki uliotiwa saini na mamlaka ya Afrika Kusini pia litashughulikiwa mjini Cape Town – mkataba unaokusudiwa kusaidia uchumi wa nchi hiyo, ambao bado unategemea sana makaa ya mawe, kuondoa kaboni, na ambayo Marekani imejiondoa.

Ukraine, DRC na Mashariki ya Kati kwenye ajenda

Kwa upande wa kidiplomasia, mkutano huo wa kilele pia utakuwa fursa ya kupitia mizozo mikuu ya kimataifa ya sasa, kuanzia vita vya Ukraine hadi mgogoro wa Mashariki ya Kati na mzozo wa mashariki mwa DRC. Katika mzozo wa Ukraine, huku Ulaya ikizidisha juhudi zake za kuungana dhidi ya Vladimir Putin, Afrika Kusini, isiyofungamana na upande wowote na mwanachama wa BRICS pamoja na Urusi, inaweza kuwa na jukumu la kutekeleza. Kama ilivyo kwa DRC, ambako, kwa ushiriki wake katika kikosi cha SADC kilichotumwa mashariki mwa nchi hiyo, tayari inashikilia nafasi kuu, wakati Mashariki ya Kati, Pretoria imekuwa moja ya sauti kuu za watu wa Palestina kwa kuwasilisha malalamiko ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israeli katika Ukanda wa Gaza mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *