
Canada imewasilisha malalamiko rasmi kwa Shirika la Biashara Dubiani dhidi ya ushuru wa forodha wa 25% uliowekwa na serikali ya Marekani kwa bidhaa zake nyingi zinazoingizwa nchini Marekai, WTO imethibitisha siku ya Jumatano Machi 5.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
“Uamuzi wa Marekani unatuacha bila chaguo lingine,” balozi wa Canada katika Shirika la Biashara Duniani lenye makao yake makuu mjini Geneva, Nadia Theodore, alisema jana Jumanne. “Nimeomba mashauriano ya WTO na serikali ya Marekani kuhusu ushuru wake usio na msingi kwa Canada,” ameandika kwenye mtandao wa Linkedin.
Siku ya Jumatano afisa wa WTO amethibitisha kuwasilishwa kwa malalamiko hayo, ambayo yanafuata yale ya China siku ya Jumanne, ambayo pia iko chini ya mfumo mpya wa ushuru wa forodha wa adhabu. Tangazo la Beijing limekuja siku moja baada ya Rais Donald Trump kutia saini agizo mpya la utendaji la kuongeza ushuru wa ziada kwa bidhaa za China hadi 20%, baada ya ongezeko la awali la 10% mwezi wa Februari ambalo tayari lilikuwa limesababisha malalamiko kutoka Beijing kwa WTO.
Bi Theodore amebainisha katika ujumbe wake kwamba alikuwa amevalia vazi la hafla hiyo na Lesley Hampton, mbunifu wa mitindo kutoka Taifa la Kwanza la “Anishinaabe na Canada”. Ishara ambayo ni sehemu ya harakati inayohimiza Wacanada kununua bidhaa za ndani badala ya za Marekani. Bi. Theodore alitia sahihi ujumbe wake kwa maneno “Elbows up,” kilio cha upinzani ambacho hutoka kwa magongo.
Hatuli tena machungwa kutoka Marekani, tunakula tufaha kutoka hapa, amesema Bi. Theodore.
Kutafuta maelewano
Kuwasilishwa kwa malalamiko hayo kunakuja wakati serikali ya Marekai ilipojitokeza Jumanne kufungua mlango wa maelewano na majirani zake wawili, Canada na Mexico, ambayo pia itakabiliwa na ongezeko la 25% la ushuru wa forodha. Katibu wa Biashara Howard Lutnick, aliyehojiwa kwenye Fox Business, ameeleza kwamba “amekuwa akizungumza kwa simu na Wacanada na Wamexico siku nzima” kabla ya kuongeza: “Rais anasikiliza (…) nadhani hatimaye atapata suluhu nao.” Kulingana na yeye, uamuzi unaweza kufanywa siku ya Jumatano.
Kuna hatua mbalimbali za kutatua mzozo katika WTO. Katika tukio la malalamiko, mashauriano yanaanzishwa kati ya wahusika. Ikiwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa, mlalamikaji anaweza kuomba kuanzishwa kwa kundi maalum, linaloundwa na wataalamu watatu, labda watano. Kisha nchi zinaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wao.
Baraza la rufaa, linaloundwa na wataalamu wa sheria na biashara za kimataifa, halijaweza kushughulikia kesi mpya tangu mwezi wa Desemba 2019 kwa sababu viti vya majaji vimesalia wazi kufuatia kuzuiwa kwa uteuzi na Marekani, zoezi lililoanzishwa chini ya utawala wa Barack Obama na kuendelea na Donald Trump na Joe Biden.