Cameroon: Watu 20 wakamatwa baada ya mauaji ya watafiti wawili kaskazini mwa nchi

Takriban siku kumi baada ya vifo vya Frédéric Mounsi na Bienvenue Bello, watafiti wawili kutoka Taasisi ya Garoua ya Utafiti wa Jiolojia na Madini ambao walikuwa wahanga wa ghasia za kiraia katika kijiji cha Mbalda, watu 20 wanaoshukiwa kushiriki katika mauaji yao walikamatwa siku ya Jumanne, Machi 11. Mamlaka za eneo hilo, kwa upande wao, ziliidhinisha kufukuliwa kwa miili ya wahanga, zoezi ambali litafanyika siku ya Ijumaa.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Yaoundé, Richard Onanena

Saa ishirini na nne baada ya kukamatwa kwao, watu 20 wanaoshukiwa kushiriki katika mauaji ya watafiti wawili kutoka Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia na Madini ya Garoua, Frédéric Mounsi na Bienvenue Bello, pamoja na mwelekezi wao, Oumarou Kalabay, kaskazini mwa Cameroon, waliendelea kusikilizwa siku ya Jumatano hii, Machi 12, kwenye jengo la askari la Mokolo.

Wakati mawakili wa familia za waaathiriwa watatu wanatumai kuwa kesi hiyo itaangazia kile kilichotokea alasiri ya Jumapili, Machi 2, katika kijiji cha Mbalda, wasomi wa jimbo la Lara, ikiwa ni pamoja na Bienvenue Bello, wanadai uchunguzi huru, hatua za kutaka utulivu kutoka kwa mamlaka, na fidia kwa wapendwa wao. Hii pia ni kesi ya chama cha maendeleo cha kijiji cha Lamé ambako Frédéric Mounsi alizaliwa, ambacho kinataka uchunguzi wa wazi na usio na upendeleo ili wale wote walio na hatia ya uhalifu huu mbaya waweze kutambuliwa.

Ufukuaji wa miili waidhinishwa

Mapema wiki hii, Wizara ya Utafiti wa Kisayansi ilisema kwamba Bienvenue Bello na Frédéric Mounsi walikuwa wamekwenda Soulede-Roua na mwelekezi wao Oumarou Kalabay kufanya utafiti kwa nia ya kutatua tatizo la upatikanaji wa maji ya kunywa linalowakabili wakazi wa Milima ya Mandara. Kuhusu vifo vya watu hao watatu, wizara ilishutumu “mauaji ya kinyama” na kutaka “haki itendeke.”

Pia siku ya Jumatano, Machi 12, viongozi wa eneo hilo waliidhinisha kufukuliwa kwa mabaki yao, kulingana na matakwa ya familia zinazoamini kuwa walizikwa kwa haraka. Familia za wahanga wataweza kuweka miili katika majeneza yaliyofungwa ili kutekeleza maziko. Mawakili wao, kwa upande wao, wanatarajia operesheni hiyo – iliyoratibiwa asubuhi ya Ijumaa, Machi 14 – kutoa vyeti vya uchunguzi wa maiti mara tu baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa watalamu wa masuala ya mifupa.

Kwa kuogopa mivutano ya jamii kufuatia janga hili, mamlaka ya jimbo la Kaskazini ya Mbali inawatolea mwito wakazi wa eneo hilo kujizuia na kutokuwa na roho yoyote ya kulipiza kisasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *