Cameroon: Paul Biya kwa mara nyingine kugombea katika uchaguzi wa urais wa 2025

Je, Paul Biya atawania kwa muhula mwingine tena katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 2025? Akiwa na umri wa miaka 92 na tayari ana miaka 43 madarakani, rais wa Cameroon anafanya siri juu ya uwezekano huu wa kugombea kwenye kiti cha urais.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Yaoundé, Polycarpe Essomba

Nchini Cameroon, wakati uvumi kuhusu nia ya Paul Biya kuwatena tena katika uchaguzi wa urais bado unaendelea kusambaa nchini, kauli hii imejiongeza kaulizingine zilizoshuhudiwa tangu hotuba zake za hivi majuzi. Mnamo Desemba 31, 2024, wakati wa hotuba yake ya Mwaka Mpya kwa taifa, rais wa Cameroon alisema kwamba “azimio lake la kutumikia nchi bado na halijabadilika.”

Siku ya Jumatano, Aprili 23, kwenye ukurasa wake wa X, amesema “anataka kuendelea kufanya kila linalowezekana ili kuendeleza mabadiliko makubwa ya kijamii na kuendelea taifa la kweli la Cameroon.” Kauli ambayo inadumisha uwezekano wa Paul Biya kuendelea kushikilia nafasi hiyo mbali na muhula wakewa sasa.

Wiki chache baadaye, katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Vijana, Paul Biya alijidhihirisha kwa mara nyingine tena kwa kusema haswa “Nitaendelea kuwa upande wenu ili kukabiliana na changamoto mnazokabiliana nazo.”

Kwa ujumbe wa hivi punde kwenye ukurasa wake wa X, Paul Biya anaondoa zaidi shaka juu ya nia yake na anaonekana kuzindua mpango wa mawasiliano katika hatua ndogo, za kimaendeleo kuelekea kutangazwa kwa yeye kugombea kwenye kiti cha urais. Ugombea ambao chama chake, RDPC, tayari kimeidhinisha. Chama hicho kimesema mara kwa mara kwamba hakina mgombea mwingine isipokuwa rais wake katika ngazi ya taifa – ambaye si mwingine ila Paul Biya. Na hii ni licha ya kutokuwa na subira iliyoonyeshwa kimya kimya na baadhi ya maafisa wa chama, ambao bado wanatumai kuwa rais atakabidhi nafasi ya kugombea kwenye kiti cha urais kwa kizazi kingine.

Hii pia ni licha ya maandamano kutoka kwa safu ya upinzani, kama vile MRC kupitia Maurice Kamto, ambaye aliona uwezekano huu wa kugombea kama “uhalifu”, au baadhi ya maaskofu wa Kanisa Katoliki ambao katika miezi ya hivi karibuni walimtaka Rais Paul Biya kuachana na azma hii.

Ikiwa imesalia chini ya miezi sita kabla ya uchaguzi wa urais, Paul Biya hivi karibuni ataweka wazi msimamo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *