Cameroon: Kiongozi wa upinzani Maurice Kamto ashutumu serikali kwa njama ya kumzuia kugombea

Nchini Cameroon, mjadala bado unaendelea kuhusu swali la iwapo Maurice Kamto atakuwa mgombea au la katika uchaguzi ujao wa urais. Katika chapisho la Jumatano, Machi 19, kiongozi huyo wa MRC alishikilia msimamo kuwa kugombea kwake ni halali kabisa na alizungumzia njama ya kisiasa na kimahakama inayolenga kumtenga na uchaguzi huo. Kiongozi huyu wa upinzani anatoa wito kwa wafuasi wake kuwa tayari. Kauli ambayo ilizua hisia nyingi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Yaoundé, Polycarpe Essomba

“MRC haitaruhusu RDPC [chama tawala] kumtenga mgombea wake kwenye kinyang’anyiro cha urais,” Maurice Kamto ameandika kwa ukamilifu katika taarifa hii. Kabla ya kusema, kwa sauti ya vitisho, “wale waliochukua uamuzi huu haramu na mikono midogo iliyohusika na utekelezaji wake wanapaswa kuukataa, kwa sababu hautafanyika bila madhara makubwa,” anaonya.

Kwa mgombea aliyependekezwa na MRC, mtu aliyehusika na njama hiyo katika maandalizi si mwingine ila Waziri wa Utawala wa Wilaya, ambaye anamtuhumu kwa “kuchukua mamlaka ya Élécam” inayohusika na kusimamia uchaguzi “na Baraza la Katiba.” Anamshutumu kwa kujipa “haki ya kuamua nani atakuwa mgombea katika uchaguzi wa urais au la.”

Majibu ya kauli ya Maurice Kamto yalitoka pale ambapo haikutarajiwa: kutoka kwa Jean de Dieu Momo, Mjumbe wa Waziri katika Wizara ya Sheria. Dieu Momo alimrithi Maurice Kamto mwenyewe katika nafasi hii, ambaye chama chake cha Paddec ni sehemu ya cha cha walio wengi bungeni, chama cha rais.

Alianza kufuta hoja zote za kisheria zilizotolewa na Maurice Kamto. Kwa mujibu wa Dieu Momo, kuna mambo mawili tu ambayo yanawezekana kwa Maurice Kamto kuwa mgombea: ama kama mgombea huru, au kama kiongozi wa chama chenye wawakilishi waliochaguliwa, zaidi ya MRC. Hali nyingine yoyote, itakuwa “maandalizi ya uasi wa kiraia kwa lengo la kuchukua mamlaka kupitia maandamano ” , anahitimisha Dieu Momo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *