Burkina Faso: Wanajeshi 21 waliopatikana na hatia ya mapinduzi yaliyofeli ya 2015 wasamehewa

Nchini Burkina Faso, takriban wanajeshi ishirini waliohukumiwa kwa jukumu lao katika mapinduzi yaliyoshindwa ya Septemba 16, 2015, walipata msamaha wa rais wiki iliyotangulia. Haya ndiyo matumizi ya sheria iliyopitishwa mwishoni mwa mwezi Desemba 2024 na wajumbe wa bunge la mpito.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kapteni Ibrahim Traoré alitia saini amri ya kuachiliwa kwa maafisa kadhaa na wasio na vyeo kutoka Kikosi cha zamani cha usalama wa rais. Kikosi cha walinzi cha rais wa zamani Blaise Compaoré, ambaye alijaribu kupindua serikali ya mpito iliyoongozwa wakati huo na Michel Kafando.

Amri hiyo ni ya Machi 24 na Kapteni Ibrahim Traoré anatoa “msamaha” kwa wanajeshi 21 wa jeshi la Burkina Faso. Watu 21 ambao wamepatikana na hatia au kufunguliwa mashitaka kwa vitendo vilivyofanywa Septemba 15 na 16, 2015. Miongoni mwa walionufaika ni maafisa sita, akiwemo Kapteni Oussène Zoumbri, afisa wa kikosi cha uingiliaji kati kutoka Kikosi cha zamani cha usalama wa rais, Luteni Relwindé Compaoré, aliyetunukiwa tuzo mara nne kwa kazi yake, Luteni Gorgo Ghislain na Abdoul Dianda, au Kapteni Goutendrini Sajenti Adama Diallo.

Kufuatia uamuzi huu, wanajeshi hawa 21 watarejelea nafasi zao ndani ya jeshi la BurkinaFaso. Lakini, amri inabainisha, “kurejeshwa huku” hakuwezi “kamwe” kutoa “nafasi zao walizokuwa wakishikilia au fidia.”

Mwishoni mwa mwaka jana, bunge la mpito lilipitisha mswada unaolenga baadhi ya watu sitini waliotiwa hatiani na mahakama ya kijeshi kwa “kuhatarisha usalama wa taifa.” Sheria hii ilitoa uwezekano kwa wale walioshiriki katika jaribio la mapinduzi ya Septemba 2015 kuwasilisha ombi la “msamaha”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *