
Nchini Burkina Faso, makumi ya wanakijiji waliuawa katika mashambulizi ya siku ya Alhamisi, Aprili 4, na kundi lenye silaha katika vijiji vya mkoa wa Sourou, magharibi mwa nchi hiyo. Wahasiriwa wengi wao walikuwa vijana waliojiunga na makundi ya watu wa kujitolea, Volunteers for the Defense of the Fatherland (VDP).
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mashambulizi hayo siku ya Alhamisi yalifanyika katika vijiji vitatu, siku chache tu baada ya operesheni ya kijeshi katika eneo hilo. Kulingana na shuhuda kadhaa zilizokusanywa, watu wenye silaha walirudi kushambulia raia baada ya jeshi kuondoka.
Watu wenye silaha walivamia vijiji vya Di, Guiedougou na Lanfiera katika mkoa wa Sourou. “Magaidi wamevamia kijiji. Wat wengi waliuawa. Idadi ya vifo inaweza kuwa karibu 200,” kulingana na manusura kutoka kijiji cha Guiedougou.
Kulingana na mtu aliyenusurika, makumi ya watu walitekwa nyara, wengi wao wakiwa vijana ambao walikuwa wamejiunga na makundi watu wakujitolea kwa Ulinzi wa Nchi ya Baba. Pia kituo cha kusukuma maji na miundombinu ya vijiji mbalimbali viliharibiwa.
Mashambulizi haya yalifanyika siku chache baada ya operesheni kubwa iitwayo “tourbillon” iliyotekelezwa na jeshi la Burkina Faso katika eneo hilo. Opereseheni hiyo iliwezesha kuwasukuma watu hawa wenye silaha kurudi kwenye mpaka na Mali.
Operesheni ambayo, kulingana na mwanakijiji moja, ingevunja “mkataba usio na uchokozi” kati ya kundi lenye silaha na raia. Kulingana na mwanakijiji huyo, wakazi wa vijiji hivyo waliwataka askari kusalia katika eneo hilo, wakihofia kulipizwa kisasi na kundi hilo lenye silaha.