Burkina Faso, Niger na Mali kuunda kikosi cha wanajeshi 5,000 kupambana na waasi

Nchi tatu zinazotawaliwa na wanajeshi katika kanda ya Sahel Afrika zimetangaza kuunda kikosi cha wanajeshi 5,000 kupambana na ghasia na harakati za makundi ya waasi ambazo zimeyakumba mataifa hayo kwa miaka kadhaa.