Burkina Faso: Mji wa Djibo bado uko kwenye tishio la wanajihadi

Kaskazini mwa Burkina Faso, Djibo ilishambuliwa tena Aprili 10. Vituo vya juu vya jeshi, vilivyoko nje ya mji, vilishambuliwa na magaidi wa JNIM. Wakazi walisikia milio mikubwa ya risasi kwa muda mrefu wa asubuhi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka mitatu, mji wa Djibo, mji mkuu wa jimbo la Soum kaskazini mwa Burkina Faso, umekuwa chini ya vizuizi vilivyowekwa na wanajihadi. Haiwezekani kwa wakazi kuingia au kutoka katika mji huo bila kulipizwa kisasi, ukatili unaofanywa na makundi yenye silaha. Hali ya kibinadamu inatisha, wakati njaa ikendelea kuwakabili wakaazi wa mji huo.

Tangu kuanza kwa vizuizi mnamo mwezi wa Februari 2022, Djibo imeonyesha changamoto za usalama zinazoikabili Burkina Faso kwa muongo mmoja. Mji huo wa kaskazini, unaojulikana kwa soko la ng’ombe, unaoshambuliwa mara kwa mara na magaidi, unakumbwa na janga la kibinadamu. Wakiwa wametengwa na maeneo mengine ya nchi, wakaazi wanatatizika kukidhi mahitaji yao ya kimsingi na nyakati nyingine wanalazimika kula majani ya miti yaliyochemshwa au kuchinja mifugo yao, ambayo ni ya thamani kwa familia nyingi.

Kizuizi kilichosababisha wahasiriwa

Katika mwaka wa kwanza wa kizuizi hicho, watoto wasiopungua wanane walikufa kwa njaa, na kusababisha wanawake mia moja kuandamana, wakiwa na vibuyu na mikebe tupu ili kuonyesha mamlaka kuwa matumbo yalikua matupu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *