
Nchini Burkina Faso, jeshi la taifa limewaangamiza washukiwa kadhaa wa kigaidi, akiwemo kiongozi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu wa kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM). Operesheni kadhaa zilifanyika wakati wa mwezi wa Februari katika mikoa kadhaa ya nchi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mnamo Februari 10, 2025, shambulio lililenga kikosi cha jeshi la Burkina Faso katika mkoa wa Sourou, magharibi mwa Burkina Faso. Vikosi vya jeshi vilijibu haraka kwa msaada wa ndege na helikopta za kijeshi.
Takriban magaidi 73 wameuawa, kulingana na televisheni ya taifa ya RTB, ikinukuu ripoti ya jeshi. Miongoni mwa magaidi waliouawa ni Djafar Libé, Abou Seydou na hasa Sangaré Kalirou, almaarufu Abdoul Kalirou, wanachama wote watatu wa kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM).
Abdoul Kalirou ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na idara za ujasusi za Burkina Faso, alishiriki katika mashambulizi kadhaa dhidi ya vikosi vya jeshi la Burkina Faso huko Toéni, Sono na Diouroum kulingana na vyanzo vya usalama. Mpiganaji huyo wa kigaidi mwenye umri wa miaka 30 anahusika katika ukatili dhidi ya raia katika majimbo ya Kossi na Sourou, kulingana na RTB.
Shirika la Habari la Burkina Faso linaripoti kwamba kuuawa kwa Abdoul Kalirou ni pigo kubwa kwa magaidi ambao bado wanafanya kazi katika eneo la Boucle du Mouhoun.