Burkina Faso: Idrissa Barry, katibu wa chama cha siasa cha Sens, atekwa nyara

Mmoja wa viogozi wa chama cha kisiasa cha Servir et non se servir (Sens), Idrissa Barry amekamatwa bila sababu yoyote rasmi na watu waliojitambulisha kama maafisa wa polisi siku ya Jumanne, Machi 18, katika makao makuu ya mji wa Saaba, viungani mwa Ouagadougou. Mapema wiki hii, Sens ilishutumu mauaji ya hivi karibuni ya raia kutoka jamii ya Fulani huko Solenzo, magharibi mwa Burkina Faso, yanayohusishwa na jeshi la BurkinaFaso na wasaidizi wake.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Alipoenda kwa ujumbe maalum katika makao makuu ya mji wa Saaba, viungani mwa Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, siku ya Jumanne, Machi 18, Idrissa Barry pengine hakutarajia kutoka akiwa amezungukwa na watu wanaojitambulisha kama maafisa wa polisi. Akikamatwa bila kibali au sababu rasmi, katibu wa kitaifa wa chama cha Servir et non se servir (Sens) ndiye mhasiriwa wa hivi punde wa tabia ambayo imekuwa kawaida kwa upande wa jeshi lililoko madarakani nchini, ambalo linataka kuwanyamazisha wale wote wanaopinga utawala wake.

Bila kuchelewa, Sens katika taarifa yake kwa vyombo vya habari “ghadhabu yake ya kina na wasiwasi wake mkubwa juu ya [….] utekaji nyara huu wa kikatili”, ikitaka “kuachiliwa mara moja na bila masharti” kwa Idrissa Barry na kuongeza kwamba “kitendo hiki cha kutoweka kwa lazima, mchana na katika jengo la utawala, kinajumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na tishio la moja kwa moja kwa sauti zote muhimu”. Bw. Barry ametekwa nyara “alipokuwa katika hadhara na rais wa ujumbe maalum katika ofisi ya mji wa Saaba,” Sens imeongeza.

Familia ya Idrissa Barry inabaini kwamba kutoweka kwake kunahusishwa na taarifa iliyochapishwa na Sens mapema wiki hii ambayo haikufurahisha utawala wa kijeshi. Katika hati hii ya Machi 14, chama hiki kilishtumu vikosi vya kuingilia haaraka na kujitolea kwa Ulinzi wa Nchi – makundi ambayo yanaunga mkono jeshi la Burkina Faso katika vita dhidi ya wanajihadi – ambayo yalifanya ukatili mbaya na wa umwagaji damu dhidi ya raia huko Solenzo mnamo Machi 11.

Kutokana na mauaji haya dhidi ya watu kutoka jamii ya Fulani wanaoshukiwa kushirikiana na wanajihadi wa Jnim, Sens inathibitisha “kwamba ikiwa ukatili wa kigaidi unapaswa kupigwa vita, hii haitatoa udhuru wa safari za kuadhibu zenye maana ya mauaji ya kimbari.” Kauli – na masharti – ambayo, kwa dhahiri, hayakufurahisha utawala wa kijeshi huko Ouagadougou.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *