
Nchini Burkina Faso, Shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch limechapisha ripoti Jumatatu, Mei 12, kuhusu mauaji yaliyofanywa na jeshi la Burkina Faso na wasaidizi wao (VDP) mwezi Machi mwaa huu huko Solenzo, katika eneo la Boucle du Mouhoun.HRW inazungumzia “mauaji ya kikabila” ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Operesheni ya Green Tourbillon 2 ilikusanya vikosi maalum vya Burkina Faso kwa wiki kadhaa, kulingana na Human Rights Watch, ambayo inashutumu jeshi na wasaidizi wake wa ndani wa VDP kulenga jamii ya Fulani.
HRW ilizungumza na mashahidi 27 kutoka Solenzo na miji kadhaa ya jirani ambayo pia ililengwa. Takriban video kumi “zinazoonyesha unyanyasaji uliofanywa na VDP dhidi ya raia wa Fulani” pia zilichunguzwa.
“Wanakijiji katika jimbo la Banwa wameelezea operesheni za kijeshi katika maeneo kadhaa kwa angalau siku sita,” ripoti hiyo imesema. VDP ilifyatua risasi hewani au kwa raia na kuiba mifugo, na kuwalazimu wanakijiji kukimbia. “Mwanakijiji amesema kuwa “VDP walitupiga risasi kama wanyama. Wanawake na watoto wengi walikufa kwa sababu hawakuweza kukimbia. “
Kulingana na shuhuda zilizokusanywa na HRW, helikopta za kijeshi na ndege zisizo na rubani zilifanya mashambulizi ya anga katika eneo hilo, zikionyesha udhibiti wa moja kwa moja wa amri ya operesheni.
Katika video zilizochambuliwa na Human Rights Watch, VDP wakitembea “kati ya makumi ya maiti” “walitoa wito wa kuangamizwa kwa watu wa Fulani.”
HRW inakumbusha kuwa, kulingana na mamlaka ya Burkina Faso, jeshi na VDP “walizuia shambulio la “kigaidi” na kuua karibu washambuliaji mia moja kabla ya kuwafuata wale waliokimbilia msituni.
Operesheni ya kijeshi iliendelea katika jimbo la Sourou ambapo, kwa mujibu wa Human Rights Watch, Jnim ilisubiri jeshi liondoke kwenda kuua dazeni kadhaa za raia ili kulipiza kisasi.