Bunge limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa mwaka 2025, ambao umeleta mabadiliko muhimu katika uongozi wa shirika hilo.
Mojawapo ya marekebisho makuu ni kuhamisha mamlaka ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC kutoka kwa waziri na kuwa chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muswada huo uliwasilishwa leo, Juni 9,2025 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Pia umeboresha masharti ya uteuzi kwa lengo la kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na ufanisi katika usimamizi wa Shirika la Nyumba.
#azamnewsupdates
Mhariri| @official_jennifersumi