Bunge la Brussels: Vita vya Israel dhidi ya Gaza ni mauaji ya kimbari

Katika hatua kubwa kwa harakati za kupigania haki za wananchi wa Palestina, Bunge la Brussels limepasisha azimio la kutambua rasmi vitendo vinavyofanywa na jeshi la Israel huko Gaza kuwa ni mauaji ya kimbari, na kutaka kuwekewa vikwazo utawala huo wa Kizayuni.