Bunge la Afrika Mashariki lasimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kwa sababu za kifedha

Bunge la nchi za Afrika Mashariki, EALA limetangaza kuwa limesimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kutokana na changamoto za kifedha, zilizosababishwa na baadhi ya nchi wanachama kushindwa kulipa michango yao ya fedha.