Brigedia Jenerali Reza Sadeghi: US imetumia dola trilioni tisa Asia Magharibi bila mafanikio yoyote

Mshauri mwandamizii wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Wamarekani hawajapata mafanikio licha ya kutumia dola trilioni tisa katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Brigedia Jenerali Hossein Reza Sadeghi, amesema kuhusu namna Wamarekani na washirika wao walivyogharimika ili kuleta machafuko katika eneo la Asia Magharibi kwamba, machafuko na njama zote zinazojiri katika eneo hili zinafanywa kwa usimamizi na uingiliaji wa Marekani; na Trump alitangaza kuwa walitumia dola trilioni saba katika eneo hili, ambazo bila shaka sasa hivi zimefikia dola trilioni tisa, lakini hawajapata mafanikio chochote.

Mshauri mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia pia kushindwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na akasema, utawala wa Kizayuni umeshindwa na Hamas na Hizbullah; na kwa mujibu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu hauwezi kurekebishika kwa namna yoyote.

Brigedia Jenerali Sadeghi ametangaza kuwa, kuangamizwa kwa utawala wa Kizayuni ni moja ya malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na akasema: ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kushinda haki dhidi ya dhulma na uonevu…/