Brazili: Rais Lula anatumai kwamba ‘haki itatendeka’ katika kesi ya Bolsonaro

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema Alhamisi kutoka Tokyo kwamba “anatumaini tu kwamba haki itatendeka” katika kesi ya rais wa zamani Jair Bolsonaro, anayetuhumiwa kwa jaribio la mapinduzi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Ikiwa Bolsonaro atapatikana hana hatia katika kesi hii, aachiliwe na atangazwe kama hana hatia. “Ikiwa atapatikana na hatia, aadhibiwe,” Lula amesema katika siku ya mwisho ya ziara yake ya serikali nchini Japani.

“Ni wazi kwamba rais huyo wa zamani alijaribu kuandaa mapinduzi nchini, ambapo alijaribu kuniua mimi na makamu wa rais (Geraldo Alckmin), na kila mtu anajua alichofanya,” Lula amesema siku ya Alhamisi katika siku ya mwisho ya ziara ya serikali nchini Japani.

Mahakama ya Juu ya Brazil ilitoa uamuzi wa kihistoria siku ya Jumatano ambao unamwacha Rais wa zamani Bolsonaro akikabiliwa na kifungo cha muda mrefu gerezani na kudhoofisha azma yake ya kurejea madarakani.

“Hana njia ya kuthibitisha kutokuwa na hatia,” Lula amesema, akiongeza kuwa ikiwa Bolsonaro “atapatikana hana hatia katika kesi hii, aachwe hana hatia. Iwapo atapatikana na hatia, aadhibiwe.”

Uamuzi huu ulichukuliwa kwa kauli moja baada ya siku mbili za mjadala, ni mshtuko katika nchi hii kubwa zaidi katika Amerika ya Kusini, ambayo bado inasumbuliwa na kumbukumbu ya udikteta wa kijeshi (1964-1985).

Jair Bolsonaro, rais wa zamani wa mrengo wa kulia (2019-2022) ambaye hakuwepo wakati wa uamuzi huo siku ya Jumatano, alikataa, mbele ya waandishi wa habari huko Brasilia, tuhuma “zito sana na zisizo na msingi”. “Inaonekana wana jambo la kibinafsi dhidi yangu,” alisema.

Akitishwa na hukumu mpya ambayo inaweza kuzidisha kufungwa kwa miaka 40 jela, alisema ni mhasiriwa wa “mateso makubwa zaidi ya kisiasa na kimahakama katika historia ya Brazili.”

Kulingana na wachunguzi, baada ya kushindwa na kabla ya kukabidhiwa madaraka, watu wanaodaiwa kula njama walifanya kazi kuandaa amri ya kutaka uchaguzi mpya ufanyike, lakini pia walipanga mauaji ya Lula, makamu wake wa rais aliyechaguliwa Geraldo Alckmin na Alexandre de Moraes, jaji wa Mahakama ya Juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *