Brazil yaishutumu US baada ya wahajiri waliofukuzwa kuwasili wakiwa wamefungwa pingu

Serikali ya Brazil imeeleza kughadhabishwa kwake baada ya makumi ya wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani kuwasili kwa ndege wakiwa wamefungwa pingu, na kusema kuwa ni “kupuuzwa waziwazi” kwa haki zao.